Mohammed Salah ashinda tuzo ya mchezaji bora

Image: GETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka huku mchezaji wa Chelsea Sam Kerr akitangazwa kuwa mchezaji bora wa kike na shirika la waandishi wa soka Football Writers' Association (FWA).

Mshambuliaji wa Misri Salah ameifungia magoli 30 Liverpool ambayo inapigania kushinda mataji matatu, ikiwemo magoli 22 katika ligi ya Uingereza.

Kerr ambaye ni raia wa Australia amefunga magoli 18 katika ligi ya wanawake ya Superleague kwa viongozi wa league hiyo Chelsea.

Salah awali alikuwa ameshinda taji hilo 2018. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Liverpool walioishinda Chelsea ili kubeba kombe la Carabao la mwezi Februari.

Kerr, 28, ndio anayeongoza jedwali la wafungaji magoli mengi katika ligi ya wanawake na ameisaidia Chelsea kufuzu katika fainali ya kombe la FA dhidi ya timu ya Manchester City.

‘’Wote Mo na Sam wamekuwa wachezaji wazuri msimu huu, walivunja rekodi za klabu na mataifa yao’’, mwenyekiti wa muungano huo wa waandishi Carrie Brown alisema.

‘’Mbali na mchezo wao mzuri uwanjani , ni viongozi na wameonesha mfano bora kwa klabu na ligi zao’’.