Simba yavunja mkataba na kocha wake Mkuu

Muhtasari
  • Vile vile Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja mkataba na kocha wa viungo Daniel De Castro Reyes

Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbii ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco Martin.

Katika kipindi chake Kocha Pablo ameiwezesha timu yetu kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi na kufika robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Uongozi wa Klabu ya Simba umeandika taarifa yake na kumshukuru Kocha Pablo kwa mchango wake ndani ya klabu hiyo.

‘’Katika kipindi chote cha kumaliza msimu kikosi chetu kitakua chini ya Kocha Msaidizi Selemani Matola’’ Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Vile vile Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja mkataba na kocha wa viungo Daniel De Castro Reyes.