Neymar anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela, Kulikoni?

Shirika la uwekezaji la Brazil linataka Neymar afungwe miaka 5 atakapofikishwa mahakama wiki ijayo.

Image: BBC

Shirika la uwekezaji la Brazil linataka Neymar afungwe miaka mitano atakapofikishwa mahakama wiki ijayo kujibu mashtaka ya ulaghai na ufisadi yanayohusiana na uhamisho wake kwenda Barcelona kutoka Santos mwaka 2013.

DIS,ambayo iliyokuwa inamiliki asilimia 40 ya haki ya mshambuliaji huyo wa ya Brazil inahoji kuwa ilipata hasara baada ya kukosa ada ya uhamishO wake unaokadiriwa ulikuwa chini

Neymar, 30, amekanusha madai hayo lakini alipoteza rufaa aliyowasilisha katika mahakama kuu ya Uhispania mwaka 2017, na kufanya kesi hiyo kufikishwa mbele ya waendesha mashtaka wa Uhispania.

Mchezaji huyo wa Paris St-Germain atalazimika kufika binafsi mahakamani siku ya kuanza kwa kesi dhidi yake mjini Barcelona Jumatatu ijayo, mahakama imesema, lakini haijabainika kama ataamrishwa kusalia mjini hu hadi kesi yote itakaposikiliszwa na kuamuliwa ndani ya wiki mbili.

Washtakiwa wengine ni wazazi wa Neymar, vilabu hivyo viwili, marais wa zamani wa Barcelona Josep Maria Bartomeu na Sandro Rosell, na rais wa zamani wa Santos Odilio Rodrigues.

Rosell pia hapo awali alikanusha makosa yoyote. Katika taarifa, Baker McKenzie, mawakili wanaowakilisha familia ya Neymar, walidai kuwa mahakama za Uhispania "hazina mamlaka ya kushtaki familia ya Neymar na kampuni yao ya N&N" kwa sababu vitendo hivyo vilifanywa na raia wa Brazil nje ya eneo la Uhispania.

Pia wanaeleza kuwa uhalifu unaodaiwa hauadhibiki nchini Brazil