Video ya Pep Guardiola akikatiza katika maoneysho ya fasheni mwaka wa 1993 yaibua vichekesho

Kwa madaha mno, Guardiola alionekana akikatiza misele kwenye jukwaa la maonyesho.

Muhtasari

• Mwanawe gwiji huyo mbunifu wa maonyesho alieleza kwamba kipindi hicho Guardiola alikuwa mchezaji wa Barcelona na aliomba nafasi ya kushirikishwa.

Katika soka la sasa, wengi wanamfahamu kocha Pep Guardiola kama mchezaji na mmoja kati ya wakufunzi wenye ufanisi mkubwa sana katika ulimwengu wa mchezo huo wa miguu kwa wanaume.

Lakini wasichofahamu wengi ni kwamba mkufunzi huyo wa timu ya Manchester City miaka ya 1990s aliwahi shiriki kama mwanafasheni wa kukatiza ulingoni kuonesha fasheni yake katika kuvaa nadhifu.

Katika video moja ambayo iliibuliwa mitandaoni, Pep enzi hizo akiwa kijana alionekana anakatiza ulingoni pamoja na wanafasheni wengine, kila mmoja akijitahidi kuonesha fasheni yake katika kuvaa nadhifu.

Kulingana na jarida la Mundual, Mbunifu wa mitindo wa Catalonia Antonio Miró aliagiza huduma ya Guardiola mchanga katikati ya miaka ya 90 alipompa Mhispania huyo jukumu la kushiriki katika moja ya maonyesho yake ya wabunifu.

Eurofoot tangu wakati huo imetoa video ya kuvutia ya onyesho la mitindo, na ni salama kusema Guardiola alikuwa rahisi machoni mwake kuhusu uanamitindo hapo zamani. Katika video, Pep anaonekana katika shati jeupe na mistari kwenye mikono mifupi na anaikamilisha kwa suruali ya kahawia iliyompwerepweta.

Jarida hilo lilisema kwamba mbunifu huyo aliyempa kazi ya uanamitindo Guardiola alifariki mwezi jana na ndio maana waliibua hadithi hiyo ambayo haijawahi zungumziwa mahali popote.

“Mapema mwezi huu, mwanamitindo wa Catalonia Antonio Miró alifariki mjini Barcelona akiwa na umri wa miaka 74. Miró, ambaye alifungua duka lake mwenyewe alipokuwa na umri wa miaka 20 tu na kuzindua lebo yake yenye jina lake mwenyewe miaka michache baadaye, alihusika na mavazi katika mwaka wa 1992 katika sherehe za ufunguzi wa Olimpiki ya majira ya joto. Mtoto wa fundi cherehani kutoka nje ya jiji, Miró aliheshimiwa kwa kutokamilika katika kazi yake na matumizi yake ya watu kutoka nje ya ulimwengu wa kitamaduni wa uundaji wa mitindo katika maonyesho yake ya miondoko…” jarida hilo ilisimulia.

"Pep alimuuliza baba yangu katika miaka ya 90 kama angeweza kuwa katika maonyesho yake", anaelezea David, "baba yangu alikuwa mfuasi wa FC Barcelona, ​​hivyo alipenda wazo hilo na akasema ndiyo."