Wachezaji wa Tottenham kuwalipa mashabiki baada ya kichapo cha 6-1 dhidi ya Newcastle

Wachezaji waliwaomba radhi mashabiki wao na kusema kama njia moja ya kudhamini mchango wao, watawafidia gharama ya tikiti zote katika mechi hiyo.

Muhtasari

• Spurs waliweka rekodi mbovu ya kufungwa mabao 5 ndani ya dakika 21 Jumapili dhidi ya Newcastle ugenini.

• "Kama kikosi, tunaelewa kuchanganyikiwa kwenu, hasira yenu. Haikuwa nzuri vya kutosha" - sehemu ya barua yao kwa mashabiki ilisoma.

Wachezaji wa Tottehnam kuwafidia mashabiki wao gharama za tikiti katika kichapo cha Newcastle.
Wachezaji wa Tottehnam kuwafidia mashabiki wao gharama za tikiti katika kichapo cha Newcastle.
Image: Twitter

Wachezaji wa Tottenham wamejitolea kufidia gharama ya tikiti za mechi kwa mashabiki waliosafiri waliohudhuria mchezo wao wa kufedheheshwa wa mabao 6-1 dhidi ya Newcastle katika taarifa ya kutatanisha.

Spurs walilala kwa mabao 5-0 ndani ya dakika 21 Uwanja wa St. James' Park Jumapili kabla ya kushindwa katika mchezo wa kihuni ulioonyeshwa na kikosi chao cha sasa. Matokeo hayo yaliifanya Spurs kumfukuza kocha wa muda Cristian Stellini mechi nne pekee baada ya kuchukua udhibiti kamili wa masuala ya kikosi cha kwanza kufuatia uamuzi wa kumtimua aliyekuwa kocha mkuu, Antonio Conte.

Kulikuwa na wito mara baada ya matokeo ya Newcastle kwa Spurs kuwarejeshea pesa mashabiki ambao walikuwa wamesafiri kwenda kaskazini kutazama timu yao ikitamba kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza, ambayo yote yanahitimisha matumaini yao ya kumaliza nne bora.

Wachezaji wa Spurs walitoa taarifa Jumanne iliyosomeka: "Kama kikosi, tunaelewa kuchanganyikiwa kwenu, hasira yenu. Haikuwa nzuri vya kutosha. Tunajua maneno hayatoshi katika hali kama hii lakini tuamini, kushindwa kama hii inauma. Tunathamini usaidizi wenu, nyumbani na ugenini, na kwa kuzingatia hili tungependa kuwafidia mashabiki gharama za tikiti zao za mechi kutoka St James' Park.”

"Tunajua hii haibadilishi kilichotokea Jumapili na tutatoa kila kitu kurekebisha mambo dhidi ya Manchester United Alhamisi jioni wakati, tena, msaada wenu utakuwa na maana kwetu. Kwa pamoja - na kwa pamoja tu - tunaweza kusonga mbele. "