Alfie Halaand: Babake Erling Halaand aliondolewa kitini baada ya kuwakera mashabiki wa Real Madrid

"Zaidi ya hayo tulilazimika kuhama kwa sababu mashabiki wa RM hawakufurahishwa na 1-1,"Alisema Alfie Halaand.

Muhtasari

•Video kwenye mitandao ya kijamii inaonekana kumuonyesha babake Erling Haaland akiwakejeli mashabiki wa nyumbani kabla ya kuondolewa katika eneo lake.

•Kiungo huyo wa zamani wa Manchester City na Leeds ni mtu wa kawaida kwenye mechi za City, ambapo mwanawe amefunga mabao 51 hadi sasa msimu huu.

Alfie Halaanda ni babake mshambuliaji wa Manchester City Erling Braut Halaand
Alfie Halaanda ni babake mshambuliaji wa Manchester City Erling Braut Halaand
Image: BBC

Alfie Haaland anasema alisindikizwa kutoka kiti chake Bernabeu kwa sababu mashabiki wa Real Madrid "hawakufurahishwa" na sherehe zake baada ya Kevin de Bruyne kuisawazishia Manchester City katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa.

Video kwenye mitandao ya kijamii inaonekana kumuonyesha babake Erling Haaland akiwakejeli mashabiki wa nyumbani kabla ya kuondolewa katika eneo lake.

Haaland alitweet: "Sawa. RM hawakufurahi tulikuwa tukisherehekea bao la KDB.

"Zaidi ya hayo tulilazimika kuhama kwa sababu mashabiki wa RM hawakufurahishwa na 1-1."

De Bruyne alifunga dakika ya 67 na kusawazisha bao la kuongoza la Vinicius Junior.

Haaland alipunga mkono kwa mikono miwili huku akitabasamu kwa umati wa watu waliokuwa chini yake, akitega masikio yake kwa mashabiki wa Real Madrid na kufanya ishara, huku ripoti nchini Uhispania zikipendekeza kuwa aliwarushia chakula wafuasi hao.

Kiungo huyo wa zamani wa Manchester City na Leeds ni mtu wa kawaida kwenye mechi za City, ambapo mwanawe amefunga mabao 51 hadi sasa msimu huu.

Miamba wa Uhispania Madrid wametwaa taji la Ligi ya Mabingwa - mashindano ambayo City bado hawajashinda - mara tano tangu 2014 na kuwaondoa mabingwa hao wa Ligi ya Premia katika hatua ya nusu fainali mwaka jana.

Mnamo Oktoba ripoti zilipendekeza kwamba kandarasi ya Haaland ina kipengele maalum cha kuachiliwa kwake ili ajiunge na Real Madrid mnamo 2024, ambayo bosi wa City Pep Guardiola alisema baadaye "sio kweli".