CR7 ajipata pabaya kwa mara nyingine akimpiga kumbo mtu aliyeomba kupiga picha naye

Mwaka jana mchezaji huyo pia aligonga na kuipasua simu ya shabiki mtoto wa Everton aliyeomba kupiga picha naye akiwa anaichezea United.

Muhtasari

• Baada ya mchezo huo Ronaldo alizidiwa na maombi ya wachezaji wa Al-Khaleej na wafanyakazi walioomba shati lake.

• Ilikuwa siku ya kufadhaisha kwa Ronaldo, huku matokeo yakififisha matumaini ya Al-Nassr kushinda taji la Saudi Pro League.

Ronaldo amsukuma vikali mtu aliyeomba kupiga picha naye.
Ronaldo amsukuma vikali mtu aliyeomba kupiga picha naye.
Image: Twitter

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na ambaye ni nahodha wa timu ya Al Nassr Christiano Ronaldo kwa mara nyingine tena amejipata kwenye utata usiofurahisha uwanjani.

Ronaldo alimsukuma mbali mshiriki wa timu ya upinzani baada ya kujaribu kupiga naye selfie kufuatia sare ya 1-1 ya Al-Nassr na Al-Khaleej.

Baada ya mchezo huo Ronaldo alizidiwa na maombi ya wachezaji wa Al-Khaleej na wafanyakazi walioomba shati lake na nyota huyo wa Ureno aliishia kumpa mchezaji mmoja.

Hata hivyo, hakuitikia kwa upole wakati mfanyikazi wa chumba cha nyuma cha Al-Khaleej alipojaribu kupiga picha naye na kuishia kumsukuma mtu huyo mbali.

Ilikuwa siku ya kufadhaisha kwa Ronaldo, huku matokeo yakififisha matumaini ya Al-Nassr kushinda taji la Saudi Pro League.

Ronaldo alifunga bao la kuotea wakati wa mchezo na timu yake ikajikuta ikiachwa kwa pointi tano na viongozi Al-Ittihad.

Tangu kuhamia kwake Al-Nassr Ronaldo amefunga mabao 12 katika mechi 13 za ligi, ingawa ripoti zinaonyesha kuwa mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or anataka kuondoka katika klabu yake hiyo mpya.

Hata hivyo, sasa inaonekana Real Madrid wako tayari kumpa Ronaldo nafasi isiyo ya kucheza kama balozi, kwa mujibu wa El Nacional.

Klabu ya Uhispania ilisema: 'Florentino Perez amehakikisha kwamba [Ronaldo] hatakosa kazi Santiago Bernabeu.

"Lakini, ni wazi, hangeweza kufanya hivyo ili kuwa mchezaji, kwa sababu anaona kuwa ni mzunguko ambao unapaswa kuzingatiwa kufungwa."

Mpenzi wa Ronaldo, Georgina Rodriguez pia anasemekana kutamani kurejea katika mji mkuu wa Uhispania ambako wanandoa hao walikutana.

Ronaldo ni gwiji wa klabu ya Real Madrid, akiwa amefunga mabao 451 katika mechi 438 wakati alipokuwa Bernabeu.