Nahisi nilidanganywa kumsaini Christiano Ronaldo - Rais wa Al-Nassr afunguka

"Katika maisha yangu nimedanganywa mara mbili, moja ilikuwa kununua kebab 3 nikaletewa mbili na nyingine ni wakati nilimsaini Ronaldo" - Al-Muammar alisema.

Muhtasari

• Mapema wiki hii, Al-Nassr walitupwa nje ya nusu-fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kuchapwa 1-0 na Al-Wehda.

• Makubaliano ya CR7 na Al-Nassr ni halali hadi msimu wa joto wa 2025, ambapo atajikusanyia takriban euro milioni 500.

Al Nassr wakana kuhusishwa na Ronaldo
Al Nassr wakana kuhusishwa na Ronaldo
Image: Marca

Cristiano Ronaldo, ambaye alijiunga na klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia katikati ya msimu, ameendelea kuwa gumzo kwa mashabiki.

Kulingana na jarida la El Desmarque, Al-Muammar, rais wa Al-Nassr, alionyesha hasira yake na uchezaji wa Ronaldo katika mahojiano na ArabiaNews50.

“Nimelaghaiwa mara mbili tu maishani mwangu. Ya kwanza ilikuwa wakati niliagiza kebab tatu na ninapokea mbili kati yao. Mara ya pili ilikuwa ni kumsajili Cristiano Ronaldo.”

Rais wa Al-Nassr alisema anahisi kudanganywa na kiwango ambacho mchezaji wa Ureno ameonyesha hadi sasa.

Ikumbukwe kwamba mabishano yamemkumba Ronaldo tangu alipowasili katika klabu hiyo ya Uarabuni, kati ya ambayo ni ishara ya kipekee aliyoitoa hadharani ikigusa sehemu zake za siri baada ya kusikia kelele za mashabiki wa Leo Messi.

Jambo hili lilisababisha hata mwanasheria wa nchi hiyo kuomba kufukuzwa kwa Mreno huyo.

Hata hivyo, chanzo kilichotajwa hapo juu kinataja kwamba mchangiaji kutoka Saudi Arabia, Achraf Ben Ayad, alieleza kuwa madai ya rais wa Al-Nassr yalitungwa na waandishi wa habari katika Arabia News 50, ambako yalijitokeza awali.

Makubaliano ya CR7 na Al-Nassr ni halali hadi msimu wa joto wa 2025, ambapo atajikusanyia takriban euro milioni 500.

Mapema wiki hii, Al-Nassr walitupwa nje ya nusu-fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kuchapwa 1-0 na Al-Wehda.

Cristiano Ronaldo alikuwa na hali ya wasiwasi katika muda wote wa mchezo.

Hali katika Al-Nassr ni ya wasiwasi sana, baada ya matokeo ya hivi karibuni. Utendaji wa nyota huyo wa Ureno haukuwa ulivyotarajiwa, na mtazamo wake hauonekani vizuri na masheikh.