Al Nassr ya Ronaldo yapigwa marufuku ya kusajili wachezaji wapya

Al Nassr, imepigwa marufuku kusajili wachezaji wapya hadi itakapomaliza kulipa deni wanayodaiwa na timu ya Leicester City.

Muhtasari

• Leicester iliwasilisha malalamiko hayo mnamo Aprili 2021 kwa sababu ya ada ya ziada ambayo hayakulipwa kutokana na mauzo ya €18m ya mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa.

• Al Nassr -- ambayo ilichukuliwa chini ya umiliki wa wengi mwezi uliopita kwa dola bilioni 700 -- bado inaweza kusajili wachezaji wapya ingawa wachezaji hao wawatweza kucheza.

Al Nassr yapigwa marufuku ya kusajili wachezaji wapya
Al Nassr yapigwa marufuku ya kusajili wachezaji wapya
Image: Al Nassr

Klabu ya Al Nassr anayochezea Cristiano , imepigwa marufuku kusajili wachezaji wapya hadi itakapomaliza kulipa deni wanayodaiwa na timu ya Leicester City, FIFA ilisema Alhamisi.

Al Nassr waliamriwa kulipa Leicester €460,000 (milioni Sh 73,056,054) pamoja na riba ya mwaka ya 5% katika uamuzi wa Oktoba 2021 na jaji aliyeteuliwa na FIFA katika kamati ya hadhi ya wachezaji wake.

Leicester iliwasilisha malalamiko hayo mnamo Aprili 2021 kwa sababu ya ada ya ziada ambayo hayakulipwa kutokana na mauzo ya €18m ya mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa mnamo 2018.

Al Nassr -- ambayo ilichukuliwa chini ya umiliki wa wengi mwezi uliopita kwa dola bilioni 700 -- bado inaweza kusajili wachezaji wapya ingawa wachezaji hao wawatweza kucheza.

"Klabu ya Al Nassr kwa sasa imezuiwa kusajili wachezaji wapya kwa sababu ya madeni," FIFA ilisema Alhamisi. "Marufuku husika yataondolewa mara moja baada ya kulipwa kwa madeni yatakayothibitishwa na wadai wanaohusika."

Usajili wa Ronaldo kama mchezaji huru mwezi Januari uliashiria mwanzo wa usajili wa wachezaji wakubwa kutoka bara Uropa na vilabu katika Ligi ya Saudia.

Al Nassr ilimsajili kiungo wa kati wa Croatia Marcelo Brozovic mwezi huu kutoka Inter Milan kwa uhamisho unaoripotiwa kuwa wa thamani ya pauni milioni 18.

Al Nassr wako nchini Ureno kwenye kambi ya maandalizi ya msimu mpya. Mnamo Agosti 22, wana mchujo wa kufuzu katika Ligi ya Mabingwa ya Asia. Al Nassr watakuwa wenyeji wa  Al Ahli au Al Wehdat .

Musa aliondoka Al Nassr yenye makao yake Riyadh mwaka 2020 na kucheza msimu uliopita akiwa na Sivasspor nchini Uturuki.