Wafahamu wanasoka wa kike waliovua jezi kusherehekea bao

Asisat Oshoala amejiunga na wanawake wengine wanne waliowahi kuvua shati uwanjani

Muhtasari

•Kuvua shati wakati mchezo wa kubumbu unaendelea huwa ni hati na wachezaji hupokea kadi za manjano wanapofanya hivyo.

Image: Asisat Oshoala// TWITTER

Baadhi ya wachezaji kabumbu wa kiume husherekea kwa kiasi kikubwa wanapofunga bao hasa bao la ushindi au bao la kusawazisha dhidi ya wapinzani wao, hata wengine hupania kuvua mashati yao wakisherekea mabao hayo kwa furaha.

Licha ya furaha yao juu, wachezaji wanovua shati uwanjani hujipata katika hatari ya kuadhibiwa kwa kupata kadi za manjano, kwani sheria za soka zinaamuru uvuaji shati wakati mechi inaendelea ni ukosaji nidhamu unaopaswa kuadhibiwa.

Katika soka ya kina dada, mambo si tofauti kwa yale ya wavulana ingawa kwa mabinti kufanya hili huwa na maswali na hisia mseto chungu nzima.

Asisat Oshoala, mwanamke mwenye uraia wa Nigeria, alifunga bao la ushindi Julai dhidi ya Australia, katika mechi ya kombe la ulimwengu kwa wanawake ambapo alisaidia timu hiyo kuicharaza Australia mabao maatu kwa mawili.

Oshoala, alijiunga na mabinti wengine wachache katika kumbukumbu za mabinti waliowahi kuvua shati kwa kusherekea wanapofunga bao kunako dakika ya 72, aliposaidia timu hiyo kujizolea alama tatu muhimu.

Katika mwaka wa 1999 finali ya kombe la ulimwengu kati ya USA na Uchina kwa wanawake, katika uga wa Rose Bowl kunazo kumbukumbu namna mwanasoka Brandi Chastain alivyosherekea.

Chastain alisherekea kwa kuvua shati lake, alipofunga bao kupitia mkwaju wa penati, ambao ambalo liitunuku USA taji la kombe la Ulimwengu kwa mara ya pili.

Sam Kerr pia anakumbukwa katika ligi ya mabingwa kwa wanawake katika ligi kuu Uingereza, alipofunga bao la ushindi katika dakika za ushei, aliposaidia Chelsea kupata ushindi dhidi ya Aston Villa.

Baadhi ya wanawake wengine ambao wamewahi kuvua mashati yao ni pamoja na Valentina Giacinti wa Ac Milan pamoja na Chloe Kelly wa Uingereza.