Caicedo: Brighton yakataa ofa ya pili ya pauni milioni 80 kutoka Chelsea ya kumnunua

Brighton walikataa ofa mbili za kumnunua kiungo huyo kutoka Arsenal mwezi Januari, na kukataa ofa ya Chelsea ya pauni milioni 70 wiki iliyopita.

Muhtasari

• Brighton & Hove Albion wameikata ofa ya pili ya zaidi ya pauni milioni 80 ya kumnunua kiungo mkabaji, Moises Caicedo kutoka kwa mahasimu wao Chelsea.

• Brighton ilimsajili Moises Caicedo kutoka klabu ya Independiente del Valle ya Ecuador kwa pauni 4.5m mwaka 2021.

Brighton yakataa ofa ya pauni milion 80 kutoka Chelsea ya kumsajili Caicedo.
Brighton yakataa ofa ya pauni milion 80 kutoka Chelsea ya kumsajili Caicedo.
Image: TWITTER

Timu ya Epl, Brighton & Hove Albion wameikata ofa ya pili ya zaidi ya pauni milioni 80 ya kumnunua kiungo mkabaji, Moises Caicedo kutoka kwa mahasimu wao Chelsea.

The Blues kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakizitafuta huduma za kiungo huyo kutoka Ecuardor kama njia ya kuboresha safu ya kati baada ya viungo zaidi ya nne kuondoka Chelsea wakati wa dirisha ya uhamisho wa msimu wa joto 2023.

Hata hivyo, mchezaji huyo anataka kuhamia klabu hiyo ya London huku akiazimia kuboresha si tu maisha yake na ya familia yake bali kuweza kubeba mataji.

Brighton ilimsajili Moises Caicedo kutoka klabu ya Independiente del Valle ya Ecuador kwa pauni 4.5m mwaka 2021.

 Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa ana thamani ya karibu pauni milioni 100 ikilinganishwa na saini ya mchezaji wa Arsenali Declan Rice ambaye alisajiliwa kwazaidi ya pauni 105 kutoka klabu ya West Ham.

Brighton walikataa ofa mbili za kumnunua kiungo huyo kutoka Arsenal mwezi Januari, na kukataa ofa ya Chelsea ya pauni milioni 70 wiki iliyopita.

Taarifa zinazofikia meza ya spoti ya Radio Jambo ni kuwa The Blues wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya mwisho kwa WanaSeaguls ya zaidi ya Pauni milioni 85 mwanzoni mwa wiki ijayo ni ikiwa ofa hiyo itakataliwa basi wataangazia macho yao kwingine.

Baadhi ya walengwa wengine ambao Chelsea watawaangazia ni pamoja na mchezaji anayewindwa na Liverpool, Romeo Lavia kutoka klabu iliyoshushwa daraja Southampton.