Moises Caicedo: Siwezi kusema hapana kwa uhamisho wa Chelsea, ni klabu nzuri

Wiki iliyopita tu Caicedo aliulizwa kuhusu Chelsea kumtaka, na akasema: "Ni kijana gani ambaye hataki timu kubwa kama Chelsea wazungumze juu yake?"

Muhtasari

• Chelsea wamemfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuwa mlengwa wao mkuu wa safu ya kati msimu huu.

• Jarida la Standard Sport linaelewa kuwa The Blues wana imani kwamba ada itashuka wakiendelea na mazungumzo na Brighton.

Akiri mapenzi yake kwa Chelsea.
Moises Caicedo Akiri mapenzi yake kwa Chelsea.
Image: Instagram

Nyota wa kulia wa klabu ya Brighton, Moises Caicedo amesisitiza hamu yake ya kujiunga na Chelsea msimu huu wa joto, akisisitiza: "Siwezi kusema hapana."

Chelsea wamemfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuwa mlengwa wao mkuu wa safu ya kati msimu huu, na wako tayari kutumia pesa nyingi kumnunua kinda huyo wa Ecuador huku Seagulls wakimpiga bei ya pauni milioni 100 kichwani.

Jarida la Standard Sport linaelewa kuwa The Blues wana imani kwamba ada itashuka wakiendelea na mazungumzo na Brighton.

Caicedo pia alikabiliwa na ofa mbili zilizokataliwa kutoka kwa Arsenal mwezi Januari na, huku Chelsea sasa wakiwa mstari wa mbele katika kuinasa saini yake, kiungo huyo alikuwa ameweka wazi kuwa anataka kuhamia London Magharibi.

"Ni timu kubwa, hiyo ni kweli," Caicedo alimwambia mwandishi wa habari wa TC Deportes, Maria Jose Flores.

"Timu ya kihistoria ambayo siwezi kukataa [kujiunga] kwa sababu ni timu kubwa sana, ya kihistoria na nzuri.

"Mji pia ni mzuri. Una kila kitu kizuri."

Wiki iliyopita tu Caicedo aliulizwa kuhusu Chelsea kumtaka, na akasema: "Ni kijana gani ambaye hataki timu kubwa kama Chelsea wazungumze juu yake?

"Najua jinsi ya kukabiliana nayo. Sichukuliwi na mihemko, nafurahiya wakati na familia yangu kwa sasa. Kuna shinikizo, lakini nimetulia.

"Ninangojea chochote atakachoamua Mungu. Atajua ni nini kilicho bora kwangu."