Hakuna mchezaji wa Chelsea aliyekubali jezi No.9 klabu ikitangaza namba za wachezaji 29

Jezi namba 9 imekuwa ikihusishwa na mikosi na wachezaji ambao walikabidhiwa jezi hiyo wote viwango vyao wa soka vilishuka baada ya kuivaa.

Muhtasari

• Chelsea mpaka sasa wana wachezaji 29 katka kikosi chao na wote wameshapokeza namba mpya za jezi zao.

• Hata hivyo, bado klabu hiyo haijatosheka katika kusaini wachezaji wapya kabla ya dirisha kufungwa mwishoni mwa mwezi Agosti.

Chelsea.
Chelsea.
Image: CHELSEA

Klabu ya Chelsea imetangaza namba za jezi za wachezaji wake 29, wakiwemo wale waliosalia na wale waliosajiliwa mpaka sasa, zikiwa zimesalia siku chache kuelekea kuzinduliwa kwa msimu 2023/24.

Klabu hiyo kupitia tovuti yao rasmi wamechapisha habari hizo zikiambatanishwa na namba ya jezi ambayo kila mchezaji amekabidhiwa.

Wachezaji kadhaa wageni na waliosalia walichagua namba mpya, wachache wakisalia namba walizokuwa nazo misimu ya nyuma.

Kwa haraka, tuliweza kubaini hakuna mchezaji hata mmoja kati ya hao 29 ambaye alikubali kuchukua jezi nambari 9 ambayo kwa muda mrfu imekuwa ikitajwa kama jezi ya mikosi na nuksi.

Jezi namba 9 imekuwa ikihusishwa na mikosi tangu enzi za wachezaji kama Fernando Torres, Romelu Lukaku, Tammy Abraham, Aubameyang miongoni mwa wengine ambao wote viwango vyao wa soka vilishuka baada ya kukabidhiwa jezi hiyo.

Hii hapa ni orodha ya wachezaji wote 29 kila mmoja na namba ya jezi aliyokabidhiwa;

1 - Kepa Arrizabalaga

2 - Axel Disasi

3 - Marc Cucurella

5 - Benoit Badiashile

6 - Thiago Silva

7 - Raheem Sterling

8 - Enzo Fernandez

10 - Mykhailo Mudryk

11 - Noni Madueke

13 - Marcus Bettinelli

14 - Trevoh Chalobah

15 - Nicolas Jackson

16 - Lesley Ugochukwu

17 - Carney Chukwuemeka

18 - Christopher Nkunku

19 - Armando Broja

20 - Andrey Santos

21 - Ben Chilwell

23 - Conor Gallagher

24 - Reece James

26 - Levi Colwill

27 - Malo Gusto

29 - Ian Maatsen

31 - Robert Sanchez

33 - Wesley Fofana

37 - Mason Burstow

47 - Lucas Bergstrom

50 - Eddie Beach

67 - Lewis Hall

Wengi wa wachezaji hao ni makinda walionunuliwa na wengine kupandishwa daraja kutoka timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18.