Kutoka Cobham hadi nahodha: Jinsi Reece James alifuata nyayo za John Terry

'Nimekuwa Chelsea maisha yangu yote. Nilianza hapa nikiwa na umri wa miaka sita na kuja kupitia Academy ni ngumu. Lakini kuendelea na kuwa nahodha, ni hisia kubwa kwangu na familia yangu.'

Muhtasari

• Mhitimu wa Cobham, Reece James atakuwa nahodha wa upande wa wanaume kuanzia sasa na kuendelea!

John Terry alivyomhimiza James
John Terry alivyomhimiza James
Image: Cheslea

Klabu ya mchezo wa miguu nchini Uingereza Chelsea wamemzindua nahodha wao mpya kuelekea msimu mpya wa soka 2023/24.

Chelsea kwa mara nyingine baada ya miaka mingi, tena wamempa kitambaa cha unahodha beki wa kulia Reece James.

James kukabidhiwa kitambaa cha unahodha ilikuwa habari kubwa kwani iliibua kumbukumbu za mchezaji wa Chelsea kati ya wachache ambao walifana kutoka academia ya vijana Cobham na kufuzu kuingia timu ya wachezaji wazima na kwenda mbele kutwaa unahodha.

Mchezaji wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni nahodha wa muda mrefu John Terry.

“Akiwa mfuasi wa utotoni wa Blues ambaye alijiunga na Academy yetu akiwa na umri wa miaka sita, Reece alikuwa chaguo bora la klabu hiyo kutuongoza ndani na nje ya uwanja msimu huu,” sehemu ya taarifa kwenye tovuti rasmi ya Chelsea ilisoma.

Mhitimu wa Cobham, Reece James atakuwa nahodha wa upande wa wanaume kuanzia sasa na kuendelea!

'Nina furaha sana kuchukua jukumu na wajibu,' alisema James. 'Najua nina viatu vikubwa vya kujaza kwa sababu tumekuwa na manahodha wakubwa hapa siku za nyuma, lakini nina furaha.’

'Nimekuwa Chelsea maisha yangu yote. Nilianza hapa nikiwa na umri wa miaka sita na kuja kupitia Academy ni ngumu. Lakini kuendelea na kuwa nahodha, ni hisia kubwa kwangu na familia yangu.'

Kocha mkuu Mauricio Pochettino alisema: ‘Huu ni uamuzi uliochukuliwa na mimi na klabu. Tunafurahi sana Reece atakuwa nahodha wa timu msimu huu.’