Mchezaji wa zamani wa Gor Mahia na Sofapaka azirai na kufariki uwanjani mechi ikiendelea

Asudi ambaye alikuwa na umri wa miaka 27 tu aliripotiwa kuanguka, kuzirai na kisha saa chche baadae kuripotiwa kuaga dunia. Anizirai uwanjani mechi ikiendelea mjini Thika.

Muhtasari

• Majaribio ya wachezaji wenzake na timu ya kiufundi ya kusimamia usaidizi wa matibabu ili kuokoa maisha yake yalishindikana.

Rafael Asudi.
Rafael Asudi.
Image: Facebook

Mchezaji wa zamani wa timu za Gor Mahia na Sofapaka Raphael Asudi ameripotiwa kuanguka, kuzirai na kufariki uwanjani wakati wa medhi mjini Thika kaunti ya Kiambu.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Asudi alikuwa anashiriki katika mechi ya kirafiki baina ya timu za Donholm Seniors dhidi ya Thika Vitambi katika uga wa Thika Municipality wakati alianguka ghafla uwanjani mechi ikiendelea na kutangazwa kufariki dakika chache baadae.

Majaribio ya wachezaji wenzake na timu ya kiufundi ya kusimamia usaidizi wa matibabu ili kuokoa maisha yake yalishindikana.

Mpaka kifo chake, Asudi alikuwa na miaka 27 tu.

“Asudi alianguka katikati ya mechi na kusababisha hofu kwa wachezaji wenzake na wapinzani. Wajumbe wa benchi la ufundi na wachezaji wenzake walijaribu kutoa huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa hospitalini. Baada ya saa mbili, ilithibitishwa kuwa mchezaji huyo amepoteza maisha,” chanzo kimoja cha habari kiliripoti.

Asudi, kulingana na chanzo cha familia, alikuwa amefanyiwa upasuaji unaohusishwa na ugonjwa wa moyo. Inasemekana aliambiwa aache soka.

Ripoti zinaonyesha kuwa mchezaji huyo alitakiwa kusafiri hadi Hungary kwa masomo mwishoni mwa mwezi baada ya kupata ufadhili wa masomo.

 

Asudi pia alichezea vilabu vingine vya Ligi Kuu ya Kenya kama Sofapaka, Nairobi Stima, Posta Rangers na Bidco United.