Jezi ya Greenwood imekuwa jezi iliyouzwa zaidi na Getafe katika kipindi cha saa 48

Mashabiki walimkaribisha Greenwood na timu kwa nderemo na mabango ya kuomba jezi yake. Alijiunga na Getafe baada ya kufukuzwa na Manchester United.

Muhtasari

• Mnamo Septemba 6, klabu hiyo ya Uhispania ilitangaza kumtambulisha fowadi huyo mwenye umri wa miaka 21.

• Rais wa Getafe, Angel Torres, pia hivi karibuni alifahamu hali ya Greenwood.

Mason Greenwood.
Mason Greenwood.
Image: X

Jezi mpya ya kinda wa Uingereza Mason Greenwood ya Getafe imekuwa jezi iliyouzwa zaidi kwenye La Liga katika kipindi cha saa 48 katika historia ya klabu hiyo kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali kutoka Uhispania.

Hii inakuja siku chini ya kumi tu baada ya mchezaji huyo aliyetemwa na Manchester United kujiunga na timu hiyo ya Uhispania.

Mnamo Septemba 6, klabu hiyo ya Uhispania ilitangaza kumtambulisha fowadi huyo mwenye umri wa miaka 21, pamoja na wachezaji wengine wawili waliosajiliwa, Diego Rico na Oscar Rodriguez, na kuwavuta zaidi ya mashabiki 5,000 waliokuwa na furaha katika uwanja wa Coliseum Alfonso.

Zaidi ya hayo, kulingana na vyanzo vingi vya habari nchini Uhispania, jezi nambari 12 ya Greenwood ikawa jezi iliyouzwa kwa kasi zaidi katika historia ya Getafe ndani ya saa 48 za kwanza baada ya kutolewa.

Baada ya kumtambulisha, kulikuwa na baadhi ya habari kwamba mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yaliitaka Getafe kufikiria mara mbili kuhusu kumsajili mchezaji huyo.

Hasa, uongozi wa klabu na mashabiki hawajajali sana kuhusu mzozo wa hivi majuzi unaomhusu kijana huyo mwenye umri wa miaka 21: "Kuwasili kwa Greenwood nchini Uhispania tangu mwanzo kuliwasisimua mashabiki wa Getafe, ambao wengi wao hawakujua au walikuwa bado hawajaelewa kwa nini alijiunga na klabu yao ndogo.

Greenwood alipofika Madrid Jumapili iliyopita akiwa na babake, mpenzi wake, na wafanyakazi wa Manchester United, aligundua kwamba angeweza kutembea mitaani bila kuvutia umakini wa watu wengi, huku watu wachache tu wakisimama kupiga picha. Rais wa Getafe, Angel Torres, pia hivi karibuni alifahamu hali ya Greenwood.

Mashabiki walimkaribisha Greenwood na timu kwa nderemo na mabango ya kuomba jezi yake. Katika sehemu ya awali ya kipindi cha mafunzo, Greenwood aliandamana na kuelekezwa na wakufunzi wawili wa mazoezi ya viungo kwa Kiingereza."

Licha ya kutocheza kwa takriban miaka miwili, wakufunzi bado wanashikilia talanta ya Greenwood kwa heshima kubwa: "Getafe imetangaza kwamba Greenwood atacheza winga, ingawa anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati.

Uongozi wa klabu na wakufunzi wanaamini kwamba Greenwood anahitaji muda kurejesha utimamu wake, kutulia katika maisha ya Madrid, lakini hawakanushi kwamba anaweza kuwa mchezaji bora zaidi kuwahi kuwahi kuwa naye katika historia.”