Malejendari wa Man Utd wafurika kumpa shavu Sir Alex Ferguson katika mazishi ya mkewe

Lady Cathy ambaye walikuwa wameoana na Ferguson kwa kipindi cha miaka 57 alifariki Oktoba 5 huko Uingereza akiwa na umri wa miaka 84.

Muhtasari

• Cathy anafahamika kuwa na mchango muhimu katika maisha ya soka ya Fergie, hasa katika kipindi cha miaka 27 kama mkufunzi wa Manchester United.

Alex Ferguson katika mazishi ya mwanawe.
Alex Ferguson katika mazishi ya mwanawe.
Image: x

Oktoba 16, mkewe aliyekuwa kocha mwenye ufanisi mkubwa kwenye timu ya Manchester United Sir Alex Ferguson, Lady Cathy Ferguson aliagwa rasmi katika safari yake duniani.

Lady Cathy ambaye walikuwa wameoana na Ferguson kwa kipindi cha miaka 57 alifariki Oktoba 5 huko Uingereza akiwa na umri wa miaka 84.

Runinga ya BBC News inaripoti kwamba malejendari wa timu ya Man Utd ambayo Ferguson alitumikia kwa miongo kadhaa walikuwa katika mstari wa mbele kusimama na mkongwe huyo wakati mgumu wa kufiwa na mtu pekee aliyekuwa karibu naye kila mara.

David Beckham na Gary Neville waliongoza magwiji wa Manchester United waliohudhuria mazishi ya mke wa Sir Alex Ferguson, Cathy.

Kulingana na BBC, wanandoa hao walioana mwaka wa 1966 na kupata watoto watatu wa kiume, akiwemo bosi wa Peterborough Darren Ferguson.

Inafahamika kwamba wapenzi hao wawili wapenzi walikutana mwaka wa 1964 walipokuwa wakifanya kazi katika kiwanda cha taipureta kabla ya Sir Alex kuanza kazi ya soka.

Cathy anafahamika kuwa na mchango muhimu katika maisha ya soka ya Fergie, hasa katika kipindi cha miaka 27 kama mkufunzi wa Manchester United.

Kwa kuzingatia ubabe wa Fergie katika soka la Uingereza, ilitarajiwa kwamba wanasoka mashuhuri wangejitokeza kwenye mazishi ya Cathy.

Gazeti la The Mirror linaripoti kwamba Beckham, ambaye alicheza chini ya Mskoti huyo huko Old Trafford, aliongoza orodha ya nyota wa zamani wa mpira wa miguu waliohudhuria safari ya mwisho ya Cathy huko Glasgow.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza alijiunga na magwiji wengine kadhaa wa United, wakiwemo Neville, Nicky, Michael Carrick, Ji-Sung Park, Bryan Robson, na Steve Bruce.

Mchezaji huyo wa Man United aliungana na gwiji wa Scotland Kenny Dalglish, kocha wa Celtic Brendan Rodgers na msaidizi wa zamani wa Rangers Archie Knox.