Cheikhou Kouyate: Mchezaji wa Senegal aondoka kambini AFCON kufuatia kifo cha babake

Kouyate tayari ameondoka Yamoussoukro na anatarajiwa mjini Dakar siku ya Jumatano kwa mazishi ya marehemu baba yake.

Muhtasari

• Kouyate, 34, ni mmoja wa wachezaji wenye uzoefu mkubwa nchini mwake akiwa na mechi 88 za wakubwa.

CHEIKHOU KOUYATE
CHEIKHOU KOUYATE
Image: Facebook

Kiungo wa kati wa Nottingham Forest, Cheikhou Kouyate amepewa ruhusa ya kurejea nyumbani Senegal kufuatia kifo cha babake Jumanne, Januari 16, 2023.

Kiungo huyo mkongwe ambaye alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Senegal dhidi ya Gambia, alielezwa kifo cha baba yake akiwa kambini na Lons of Teranga.

Kouyate tayari ameondoka Yamoussoukro na anatarajiwa mjini Dakar siku ya Jumatano kwa mazishi ya marehemu baba yake.

Kouyate, 34, ni mmoja wa wachezaji wenye uzoefu mkubwa nchini mwake akiwa na mechi 88 za wakubwa.

Shirikisho la Soka la Senegal lilitoa taarifa kufuatia habari hiyo, na kuthibitisha kwamba mkongwe huyo ameruhusiwa kurejea Dakar.

Kiungo huyo ambaye hapo awali alicheza soka ya Ligi Kuu ya Uingereza katika klabu za West Ham United na Crystal Palace, alikuwa mbadala wa mechi ya kwanza ya kundi la Senegal.

Vijana wa Aliou Cisse walipata ushindi mzuri wa 3-0 dhidi ya Gambia yenye wachezaji 10, huku Lamine Camara akifunga mara mbili.

“Rais wa Shirikisho la Soka la Senegal Bw Augustin Senghor, wajumbe wa kamati ya utendaji, kocha wa timu ya taifa ya kandanda Bw Aliou Cisse, wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda na familia ya mpira wa miguu wana majuto na uchungu mkubwa kuwataarifu juu ya kifo cha Bw Bangiougou Kouyate, babake Cheikhou Kouyate, mchezaji wa timu ya taifa ya Senegal,” taarifa hiyo ilianza kwa mujibu wa Mirror.

"Kifo chake kilitokea Jumanne hii, Januari 16, huko Dakar. Mazishi yamepangwa kufanyika Jumatano Januari 17 katika msikiti wa Khar Yalla na kufuatiwa na maziko katika makaburi ya Musalman huko Yoff.

 

"Katika hali hii chungu, Shirikisho la Soka la Senegal linawasilisha rambirambi zake za kusikitisha zaidi kwa Cheikhou Kouyate ambaye pia aliidhinishwa kuondoka kwenye mkutano wa timu ya taifa leo, kwenda kwenye mazishi huko Dakar."