Andre Onana: Nembo ya 'mablanda' kutoka ngazi za klabu hadi kwenye timu ya taifa

Wengi walihisi kwamba makosa ambayo amekuwa akiyafanya katika mechi ya klabu yake ya Manchester United ndio yale yale ambayo yalijidhihirisha katika mecho yake kwenye timu ya taifa.

Muhtasari

• Mapambano ya kipa huyo yaliendelea, akipoteza pasi rahisi na kuachia kiki ambalo lilisababisha kurushiana maneno makali na beki.

• Cameroon walijikuta wakiachwa nyuma kwa bao moja, na mwanzo wa Onana ulikua ishara ya shinikizo kubwa kwa kipa huyo mwenye kipawa.

ANDRE ONANA
ANDRE ONANA
Image: X

Kwa mara nyingine tena mlinda lango wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Cameroon, Andre Onana amejipata kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufanya makosa yanayoweza kuepukika katika mechi yake ya kwanza kwenye timu ya tiafa katika michuano ya AFCON Makala ya 2024.

Mechi ya kwanza ya Onana ilichukua zamu isiyotarajiwa aliposhindwa kudaka mpira wa angani, na kuipa Senegal faida ya mapema ndani ya dakika 16 za kwanza.

Hili lilimfanya Onana asimame kwenye nafasi yake huku Ismaila Sarr wa Senegal akitumia makosa na kumaliza mpira wa kona na kuutusha wavuni.

Kosa hilo liliweka sauti kwa kile ambacho kingekuwa utendaji wa kutatanisha, kwa kizuia mpira huo.

Mapambano ya kipa huyo yaliendelea, akipoteza pasi rahisi na kuachia kiki ambalo lilisababisha kurushiana maneno makali na beki.

Cameroon walijikuta wakiachwa nyuma kwa bao moja, na mwanzo wa Onana ulikua ishara ya shinikizo kubwa kwa kipa huyo mwenye kipawa.

Lions of Teranga walidhibiti kipindi cha pili walipomaliza kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuongeza bao lao mara mbili.

Mchezaji wa Cameroon Jean Charles Castelleto aliifungia Senegal bao la kufuta machozikunako dakika ya 83 kabla ya Senegal kumaliza udhia kwa kuongeza bao la tatu ambalo lilionekana kama smumari wa mwisho kwenye jeneza la Wakameruni.

Licha ya uboreshaji fulani katika uchezaji wake wa kisanduku, ikithibitishwa na ngumi zilizofanikiwa kuondoa krosi zilizofuata, shaka iliendelea katika uchezaji wa Onana.

Makosa haya yalimvuta Onana mitandaoni, baadhi ya mashabiki wa soka wakimsuta vikali kwa kuipa Senegali zawadi ya bao la kwanza ambalo angelizuia.

Wengi walihisi kwamba makosa ambayo amekuwa akiyafanya katika mechi ya klabu yake ya Manchester United ndio yale yale ambayo yalijidhihirisha katika mecho yake kwenye timu ya taifa.