Morocco waibuka na hoja tata kuhusu rais wa CAF kuhudhuria mechi za Afrika Kusini zote

Ikumbukwe Motsepe ni raia wa Afrika Kusini, na jarida la Morocco sasa linadai kwamba rais huyo wa CAF kuhudhuria katika mecho zote za Afrika Kusini kunachangia wao kushinda hadi kutinga robo fainali.

Muhtasari

• Motsepe alihudhuria mechi zote mbili za mtoano za Bafana wiki jana, kwanza alisafiri hadi San Pedro kwa mechi ya timu hiyo dhidi ya Morocco.

• Na kisha kwenda Yamoussoukro kwa pambano la robo fainali dhidi ya Cape Verde.

Patrice Motsepe
Rais wa CAF// Patrice Motsepe
Image: CAF//X

Baada ya kushindwa katika mchezo wa miguu na kubanduliwa kwenye dimba la AFCON nchini Ivory Coast, Morocco sasa wameanza mchezo wa midomo wakiibua maswali yenye utata kuhusu rais wa CAF, Patrice Motsepe kuhudhuria mechi zote za Afcon ambazo Afrika Kusini inashiriki.

Ikumbukwe Motsepe ni raia wa Afrika Kusini, na jarida moja la Morocco sasa linadai kwamba rais huyo wa CAF kuhudhuria katika mecho zote za Afrika Kusini kunachangia wao kushinda hadi kutinga robo fainali.

Kwa mujibu wa jarida la GOAL.com Africa, Chapisho hilo linaangazia kwamba waangalizi kadhaa, ikiwa ni pamoja na wachambuzi, wana wasiwasi kuhusu ushawishi unaoweza kutokea wa mahudhurio ya mzee huyo wa miaka 62 kwenye maamuzi yaliyotolewa na waamuzi wa uwanjani na maafisa walioteuliwa wa VAR wakati wa mechi.

"Wengi wa wale wanaovutiwa na Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast na wachambuzi wa michezo walibaini kuwa Rais wa Caf (Patrice) Motsepe huhudhuria mechi nyingi za timu ya taifa ya Afrika Kusini, na kujiuliza kama kuhudhuria kwake kulikuwa kwa makusudi," ilisema kwenye tovuti ya Morocco SATV.ma

“Pamoja na tofauti ya uhamaji kutokana na uchezaji wa timu yake katika viwanja kadhaa, baada ya kuhamia San Pedro kumenyana na Morocco na kutoka mji wa Yamoussoukro kumenyana na Cape Verde, jambo ambalo liliwafanya wafuasi wengi kuona uwepo wake unaweza kuweka shinikizo kubwa kwa waamuzi wa uwanjani na watawala, na hivyo kushawishi maamuzi yao, jambo ambalo linaweza kuutoa mchezo katika asili yake ya kimichezo,” ilihitimisha ripoti hiyo.

Motsepe alihudhuria mechi zote mbili za mtoano za Bafana wiki jana, kwanza alisafiri hadi San Pedro kwa mechi ya timu hiyo dhidi ya Morocco, na kisha kwenda Yamoussoukro kwa pambano la robo fainali dhidi ya Cape Verde.

Hata hivyo, afisa mmoja wa Umoja wa Afrika aliliambia gazeti la Al Arab kwamba uwezo wa Motsepe kuhudhuria mechi katika miji tofauti umerahisishwa na matumizi yake ya ndege ya kibinafsi, inayomruhusu kutazama michezo mingi kwa siku moja.