Leicester yasherehekea birthday ya aliyekuwa mwenyekiti wao Vichai Srivaddhanaprabha aliyefariki 2018

Khun Vichai Srivaddhanaprabha aalikuwa mfanyabiashara bilionea wa Thailand na mwanzilishi, mmiliki, na mwenyekiti wa King Power na klabu ya soka ya Leicester, mabingwa wa EPL 2017.

Muhtasari

• Srivaddhanaprabha, bilionea wa Thailand alifariki 2018 baada ya ndege yake ya kibinafsi kupata hitilafu angani na alikuwa na umri wa miaka 60.

• Tarehe 27 Oktoba 2018, helikopta ya Vichai ilianguka nje ya Uwanja wa King Power muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanjani.

Khun Vichai Srivaddhanaprabha
Khun Vichai Srivaddhanaprabha
Image: FACEBOOK..LEICESTER CITY

Klabu ya soka inayoshiriki ligi ya Championship nchini UIngereza, Leicester City leo Aprili 4 inasherehekea siku ya kuzaliwa ya aliyekuwa mwenyekiti wao Vichai Srivaddhanaprabha ambaye alifariki 2018 kwa ajali ya ndege.

Srivaddhanaprabha, bilionea wa Thailand alifariki 2018 baada ya ndege yake ya kibinafsi kupata hitilafu angani na alikuwa na umri wa miaka 60.

Kupitia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii, Leicester City waliamsherehekea wakisema ingekuwa siku yake ya kuzaliwa kufikisha miaka 66.

“Leo ni siku ya kuzaliwa ya 66 ya mwenyekiti mpendwa wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha,” Leicester walisema wakiambatanisha na picha ya bilionea huyo marehemu.

Khun Vichai Srivaddhanaprabha aalikuwa mfanyabiashara bilionea wa Thailand na mwanzilishi, mmiliki, na mwenyekiti wa King Power.

Alikuwa mmiliki wa timu ya Premier League ya Leicester City kuanzia 2010 hadi kifo chake katika ajali ya helikopta kwenye Uwanja wa King Power wa klabu hiyo mwaka 2018.

Katika umiliki wao, alishuhudia timu hiyo ikiandikisha historia kwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Premier mwaka 2017, miaka michache baada ya kupandishwa ngazi kutoka Championship.

Tarehe 27 Oktoba 2018, helikopta ya Vichai ilianguka nje ya Uwanja wa King Power muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanjani.