Mustakabali wa VAR kuamuliwa kupitia kura baada ya pendekezo la wolves

Wolves wapokeza malalamishi kuhusu VAR kwa wasimamizi wa ligi kuu ya Uingereza.

Muhtasari

•Vilabu vya ligi kuu ya Uingereza kupiga kura kuhusu mustakabali wa VAR.

•Wolves wapokeza malalamishi yao kuhusu  VAR.

VAR
VAR VAR
Image: HISANI; Facebook

Vilabu vya ligi kuu ya  Uingereza vinatazamiwa kupiga kura kuhusu mustakabali wa VAR katika mkutano wao mkuu wa mwaka mwezi ujao, baada ya pendekezo la kufuta mfumo wa waamuzi wasaidizi wa video kuwasilishwa na klabu ya wolves.

Wolves waliwasilisha rasmi pendekezo lao kwa Ligi Kuu ya Uingereza, wakitaka VAR itupiliwe mbali msimu huu wa joto . Kutakuwa na fursa kwa vilabu vyote 20 kupiga kura kwa ajili ya au dhidi ya VAR watakapokutana mjini Harrogate mnamo Juni 6.

VAR imetumika katika ligi kuu ya Uingereza tangu 2019 lakini imekuwa na utata .Msimu huu ukishuhudia matukio mengi yanayosababisha ukosoaji mkubwa wa michakato inayohusika. Timu zingine zimetilia shaka uadilifu wa mashindano kwa sababu yake.

Taarifa ya Wolves ilisema:

“Kuanzishwa kwa VAR mwaka wa 2019/20 ilikuwa uamuzi uliotolewa kwa nia njema na kwa maslahi ya soka na Ligi Kuu moyoni mwake. Hata hivyo, imesababisha matokeo mabaya mengi yasiyotarajiwa ambayo yanaharibu uhusiano kati ya mashabiki na soka, na kudhoofisha thamani ya chapa ya Ligi Kuu.

Uamuzi wa kuwasilisha azimio hilo umekuja baada ya kutafakariwa kwa kina na kwa heshima kubwa kwa Ligi Kuu, PGMOL na washindani wenzetu. Hakuna lawama ya kulaumiwa - sote tunatafuta matokeo bora zaidi kwa kandanda - na washikadau wote wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii kujaribu kufanya kuanzishwa kwa teknolojia ya ziada kufanikiwa.

Walakini, baada ya misimu mitano ya VAR katika Ligi Kuu ni wakati wa mjadala wa kujenga na muhimu juu ya mustakabali wake. Vilabu vyote vya madaraja ya juu vina haki ya kikatiba kuwasilisha pendekezo lolote wanaloona ni muhimu kwa Ligi Kuu na zinahitaji wingi wa theluthi mbili ili kupitishwa...'

Bodi ya sasa ya Ligi Kuu ya Uingereza haioni kuwa hii ndio njia sahihi na inaamini kuwa kuondoa VAR kutaongeza maamuzi yasiyo sahihi kwenye mchezo. Pia inafikiri pengo lililosalia, baada ya kuondolewa kwa VAR, kunaweza kuweka ukosoaji mkubwa zaidi kwenye maamuzi ya uwanjani yanayofanywa na wasimamizi wa mechi na kuongeza kufadhaika kwa wafuasi.

Ligi hiyo inaelekeza kwenye ubunifu kama vile teknolojia ya kuotea ya nusu-otomatiki  na matangazo ya VAR ya uwanjani kama ushahidi wa juhudi zinazofanywa kuboresha mfumo. Tangu VAR kuletwa miaka mitano iliyopita, idadi ya maamuzi sahihi yaliyofanywa katika michezo imeongezeka kutoka asilimia 82, kabla ya kuanzishwa kwake, hadi asilimia 96 msimu huu.