Hisia mseto baada ya utabiri wa zamani wa Mnigeria kuhusu jinsi Arsenal itashinda ligi kuibuka

Kufikia sasa, utabiri wa Ifeoluwani unaonekana kuwa kweli.

Muhtasari

•Ifeoluwani alitabiri kwamba Arsenal watakuwa nyuma ya City kwa pointi mbili kabla ya mechi ya mwisho lakini wangeshinda kombe hilo.

•Ligi Kuu ya Uingereza, msimu wa 2023/24 itafikia tamati Jumapili ya Mei 19, 2024.

 

Image: TWITTER

Tweet ya zamani ya shabiki wa soka wa kike wa Nigeria ikizungumzia jinsi Arsenal ingetwaa taji la EPL 2023/24 inavuma hivi sasa kwenye mtandao huo wa kijamii.

Mnamo Desemba 4, 2023, mtumiaji wa twitter anayejitambulisha kama Ifeoluwani alitabiri kwamba Arsenal watakuwa nyuma ya Manchester City kwa pointi mbili kabla ya mechi ya mwisho ya EPL mnamo Mei 19,2024 lakini wangeshinda kombe hilo baada ya vijana wa Pep Guardiola kupoteza mechi yao ya mwisho.

Alitabiri kuwa City wangepigwa na mpinzani wao huku wanabunduki wakishinda kufuatia bao la beki Gabriel katika dakika za mwisho.

"Nilisema mapema kwenye kundi la arsenal mwanzoni mwa msimu, kwamba niliota kwamba Arsenal walikuwa nyuma ya Citykwa pointi 2 kabla ya mchezo wa mwisho wa msimu. Kisha City walipoteza mechi yao huku tukipata bao la kichwa la dakika za mwisho kutoka kwa Gabriel na kutushindia mchezo wetu wa mwisho na taji la ligi. Niite mwendawazimu o😂😂,” Ifeoluwani aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Twiti hiyo iliyochapishwa zaidi ya miezi mitano iliyopita imefufuliwa huku EPL ikiwa katika wiki ya mwisho huku Man City wakiwa kileleni mwa jedwali, wakiwa mbele ya Arsenal wakiwa na pointi mbili pekee.

Kufikia sasa, utabiri wa Ifeoluwani unaonekana kuwa kweli. Lakini je, utabiri wake kuhusu siku ya mwisho ya ligi utabainika kuwa kweli? Naam, itabidi tungojee hadi Jumapili ili kudhibitisha ikiwa aliota sawa au vibaya.

Tazama maoni ya baadhi ya mashabiki wa soka kwenye Twitter;

Mel Moore: You have given me hope beyond measure.

Slump God: Nangojea Sunday nione huu muujiza.

Big Poppa: Your prophesy is half there. Let’s wait and see if the other half will materialize on Sunday.

Marvine: I refuse this dose of hope. I have already accepted our fate.

Abdul: Walahi, if this tweet comes to pass. She is definitely going places.

Damola Agbomola: As an Arsenal fan, I hold on tenaciously to this!!!

Ligi Kuu ya Uingereza, msimu wa 2023/24 itafikia tamati Jumapili ya Mei 19, 2024.

Manchester City ambao kwa sasa wanaongoza jedwali wakiwa na pointi 88 watacheza dhidi ya West Ham katika Uwanja wa Etihad huku Arsenal walio nambari mbili na pointi 86 wakiwakaribisha Everton katika uwanja wa Emirates siku hiyo hiyo.