Sababu ya Reece James kufungiwa mechi 4 badala ya 3 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu

Mchezaji wa Manchester United Casemiro (msimu uliopita) na Yves Bissouma wa Tottenham Hotspur (msimu huu) ni baadhi ya wachezaji wengine ambao wamekumbwa na sheria hii.

Muhtasari

• Licha ya kutumikia muda mwingi nje ya uwanja kutokana na jeraha, Muingereza huyo alirejea wikendi jana baada ya takribani miezi 6 nje na kuonyesha mchezo mzuri.

Reece James kuwa nje hadi Machi.
Reece James kuwa nje hadi Machi.
Image: CHELSEA

Sasa ni rasmi kwamba nahodha wa Chelsea, Reece James atakosa mchuano wao wa mwisho kufunga msimu nyumbani dhidi ya Bournemouth na pia kukosa mechi 3 za kufungua msimu ujao baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.

James ambaye aliingia kama nguvu mpya katika mpambano wao ugenini dhidi ya Brighton alionyeshwa kadi nyekundu, dakika 20 tu baada ya kuingia uwanjani.

Licha ya kutumikia muda mwingi nje ya uwanja kutokana na jeraha, Muingereza huyo alirejea wikendi jana baada ya takribani miezi 6 nje na kuonyesha mchezo mzuri.

Lakini maonyesho yake yaliingia doa wakati wa mechi dhidi ya Brighton ambapo alionyeshwa nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa wa Brighton, Joao.

Nyekundu hiyo inamaanisha kuwa ni yake ya pili, kufuatia nyekundu nyingine aliyoonyeshwa mwaka jana katika mechi dhidi ya Newcastle, na kumaanisha atafungiwa mechi 4 mfululizo za ligi ya premia.

Kwa mujibu wa sheria za ligi ya premia, mchezaji akipata kadi nyekundu mara mbili kwa msimu mmoja, katika adhabu ya kadi nyekundu ya pili, atalazimika kukosa mechi 4 badala ya 3 katika hali ya kawaida ya nyekundu moja.

"Kwa kila kadi nyekundu ya ziada inayopokelewa katika msimu wa kucheza, mchezaji atapokea adhabu ya ziada ya kusimamishwa kwa mchezo mmoja juu ya kusimamishwa kiotomatiki."

Mchezaji wa Manchester United Casemiro (msimu uliopita) na Yves Bissouma wa Tottenham Hotspur (msimu huu) ni baadhi ya wachezaji wengine ambao wamekumbwa na sheria hii.