Kevin Omondi atuzwa kama mlinda lango bora FKF

Kipa wa Gor Mahia,Kevin Omondi ashinda glavu ya dhahabu zikiwa zimesalia mechi 4 kabla ya ligi kutamatika.

Muhtasari

•Omondi kutawazwa mshindi wa glavu ya dhahabu.

•Mechi nne zimesalia kabla ya FKF kutamatika

Kipa wa Gor Mahia;Kevin Omondi
Kipa wa Gor Mahia;Kevin Omondi

Mlinda lango wa timu ya Gor Mahia , Kevin Omondi atakabidhiwa tuzo ya glavu ya dhahabu kwenye ligi kuu ya Kenya.

Mlinzi huyo wa zamani wa Sofapaka alimaliza mchezo wa Alhamisi 16 Mei,2024  dhidi ya KCB bila kufungwa bao.Kwa sasa Omondi hajafungwa kwa mechi kumi na nane, kihesabu hakuna mlinda lango mwingine atakayempita.

Mpinzani wake wa karibu Patrick Matasi,ameachwa kwa umbali.Matasi hajafungwa kwa mechi 13.kwa mechi nne zilizosalia,hawezi kumfikia Omondi.

Msimu uliopita,Omondi hakufungwa kwa mechi sita akiwa Sofapaka.Omondi amempita Gad Matthews kwa kulinganisha msimu uliopita  baada ya Matthews kutofungwa kwa mechi 17 pamoja na mlinzi wa

Kipa huyo aidha, alirejea kwenye kikosi cha kwanza cha Gor Mahia, baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye  debi la mashemeji

Zikiwa zimesalia mechi nne katika Ligi Kuu ya FKF,Gor Mahia wako kwenye mkondo thabiti wa kuvuka alama 70 walizopata msimu uliopita. Kwa sasa wanaongoza jedwali wakiwa na alama 64 wako alama tisa mbele ya Kenya Police FC iliyo nafasi ya pili. Ushindi mmoja kutoka kwa mechi zao zilizosalia utawahakikishia taji lao la 21 la ligi na kudhihirisha tena ubabe wao katika soka la Kenya.