Southampton yarejea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza

Southampton waliwashinda Leeds 1-0 kwenye mechi ya mchujo iliyochezwa ugani Wembley JUmapili 26.

Muhtasari

• Bao lake Adam Armstrong liliwawezesha Southampton kujiunga na Leicester City  pamoja na Ipswich town kwenye ligi kuu ya Primia.

•Watapokea malipo ya angalau pauni milioni 140 huku kukiwa na uwezekano wa kupanda hadi pauni milioni 305 ikiwa wataepuka kushushwa daraja msimu ujao.

Wachezaji wa Southampton wakisherehekea baada ya bao la Armstrong picha;Instagram
Wachezaji wa Southampton wakisherehekea baada ya bao la Armstrong picha;Instagram

Southampton imerejea kwenye Ligi ya Premia kwa kuwalaza Leeds United 1-0 katika fainali ya mchujo ya ubingwa kwenye uwanja wa Wembley siku ya Jumapili.

Mshambuliaji Adam Armstrong ndiye aliyeshindia Southampton mechi hiyo kwani bao lake la kipindi cha kwanza lilitosha kuwaondoa Leeds ambao walijitahidi kupata ushindi, huku mchezaji wa akiba Daniel James akikaribia zaidi shuti lake lilipogonga lango mwishoni mwa kipindi cha pili.

Southampton inajiunga na washindi wa Championship Leicester City na mshindi wa pili Ipswich Town kupanda katika Ligi ya Primia msimu ujao. Ipswich ilipandishwa daraja baada ya kukosekana kwa miaka 22 kwenye ligi kuu.

Southampton walipata bao muhimu baada ya dakika ya 24 wakati Armstrong alipounganishwa  mpira uliochongwa na Will Smallbone na kumpita kipa Illan Meslier kwa bao lake la 24 msimu.

Kurejea kwa Southampton kunamaanisha kuwa watapokea malipo ya angalau pauni milioni 140, kulingana na uchambuzi kutoka kwa Kikundi cha Biashara cha Michezo cha Deloitte. Hii inaweza kupanda hadi zaidi ya pauni milioni 305 ikiwa kikosi cha Martin kitaepuka kushushwa daraja baada ya msimu wao wa kwanza kurejea ligini Deloitte alisema.

'Ninahisi furaha sana. Ninahisi kuzidiwa na upendo na usaidizi ambao nimekuwa nao," bosi wa Southampton, Russell Martin alisema.

Martin, ambaye alicheza chini ya meneja wa Leeds Daniel Farke kule Norwich City, alichukua tu hatamu mwanzoni mwa msimu kufuatia kuteremka daraja kwa Saints kutoka Ligi ya Primia. Sasa atasimamia ligi kuu kwa mara ya kwanza baada ya kucheza huko Swansea City na MK Dons.