VAR kuendelea kutumika katika ligi kuu ya Uingereza (EPL)

Vilabu vya ligi kuu ya Uingereza vimepitisha kusalia kwa VAR baada ya kura kufanyika Alhamisi 6,Juni 2024

Muhtasari

•Vilabu vya ligi kuu ya Uingereza vimepiga kura na kuidhinisha VAR kusalia japo marekebisho kidogo yafaa kuangaziwa

•Wolves walianzisha hoja ya VAR kuondolewa baada ya msururu wa maamuzi ya VAR kuwakandamiza msimu uliopita.

VAR
VAR
Image: HISANI

Vilabu vingi vimeonyesha nia ya kuona maboresho yakifanywa kwa mchakato wa VAR, badala ya kuondolewa kabisa kwa teknolojia hiyo.

Wolves walikuwa wameongoza msukumo wa kufuta mfumo huo baada ya msururu wa makosa, lakini katika kura ya Alhamisi, uamuzi ulifanywa  huku kura ikionyesha kutofutiliwa mbali kwa VAR.

"Kama sehemu ya majadiliano ya kina katika mkutano mkuu wa mwaka, ilikubaliwa kuwa PGMOL, Ligi Kuu na vilabu vyote vina majukumu muhimu ya kutekeleza...:' Taarifa ilisema.

Ligi ya Premia imekuwa kwenye shinikizo kubwa la kutaka kurekebisha VAR, ambayo ilianzishwa mwanzoni mwa msimu wa 2019.

Aidha ,2024 kutakuwa na utekelezaji wa teknolojia ya kuotea ya nusu otomatiki, ambayo imeundwa ili kuharakisha mchakato wa VAR na kupunguza uwezekano wa makosa.

Pia kuna mipango ya utangazaji wa moja kwa moja wa video na sauti za maamuzi ya VAR ili kuhakikisha watazamaji wanafahamishwa kuhusu michakato inayoendelea.

Matangazo ya ndani ya mchezo, ambayo yalitumika wakati wa Kombe la Dunia la wanawake 2023, yatawaruhusu waamuzi kuelezea maamuzi ya baada ya VAR kwa wafuasi kwenye viwanja.