Engin Firat asema ana mfumo wake wa kucheza dhidi ya Cameroon

Firat asifia wachezaji wake kwa ushundi wa jana dhidi ya Namibia

Muhtasari

• Harambee stars ilipata ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Namibia katika mechi yao ya kundi J ya kufuzu AFCON mwaka wa 2025

• Kocha Engin Firat amelalamikia kutolipwa mshahara wa miezi tisa licha ya kufanya vyema na wachezaji wake.

Kocha Mkuu wa Harambee Stars Engin Firat.
Kocha Mkuu wa Harambee Stars Engin Firat.
Image: Maktaba

Kocha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Engin Firat amesema ana mfumo wake atakaotumia kucheza dhidi ya miamba wa soka barani Afrika Cameroon.

Harambee Stars ilipata ushindi wake wa kwanza jana Jumanne dhidi ya Namibia kwenye mchuano ya kufuzu AFCON ya mwaka 2025.

Firat amesifia wachezaji wake kwa ushundi wa jana licha ya kukosa vifaa na sehemu maalum ya kufanyia mazoezi. Firat pia amesema anakosa kikosi kamili cha kucheza nacho kwani wengi wa wachezaji wa kikosi cha kwanza wana majeraha mbali mbali.

Firat aidha amewataka mashabiki wa Kenya kuwa watulivu kwani ana mfumo wake wa kucheza atakaotumia dhidi ya Cameroon.

Katika mechi ya kwanza waliocheza na Zimbabwe, kocha Firat alipata kashfa kutoka kwa mashabiki kwa kutopata ushindi  mechi ya nyumbani. Mashabiki walilalama kuwa mfumo wa Firat wa kucheza bila washambulizi ni bure kabisa.

Vile vile kocha amewasifia wachezaji kwa kutambua lengo lao uwanjani na kupata ushindi muhimu akisema kufikia sasa hawajapoteza mechi licha ya kucheza ugenini na mbali na nyumbani.

Licha ya kuwahongera wachezaji kwa ushindi wa kihistoria dhidi ya Namibia, Firat amelalamika kuwa hajalipwa mshahara wa miezi tisa iliyopita.

Kufikia sasa, Stars wanaongoza jedwali la kundi J kwa alama nne wakifuatiwa na Cameroon kwa alama sawia.

Mabao ya Stars ya mechi ya jana walifungwa na John Avire katika dakika ya 58 na Duke Abuya dakika ya 76. John Avire alifunga bao lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza kuchezea timu ya taifa.

Harambee Stars watacheza dhidi ya Cameroon mechi ya tatu mnamo tarehe 7 Oktoba mwezi huu.

Kocha Mkuu wa Harambee Stars Engin Firat.
Kocha Mkuu wa Harambee Stars Engin Firat.
Image: Maktaba