Mataifa ya Afrika mashariki yajikakamua michuano ya kufuzu AFCON 2025

Timu za mataifa ya Afrika Mashariki zaongoza makundi ys mechi za kufuzu AFCON

Muhtasari

• Kenya, Uganda na Tanzania zipo katika nafasi nzuri ya kufuzu kipute cha AFCON ya mwaka 2025 kufikia sasa.

• Mataifa mengine ya ukanda mpana wa Afrika Mashariki ikiwemo Sudan Kusini na DR Congo pia zinashikilia nafasi nzuri katika jedwali ya makundi

Image: Hisani

 

Timu za taifa za nchi kutoka ukanda mpana wa Afrika mashariki zimeonyesha ueledi katika michuano inayoendelea ya kusaka nafasi ya kushiriki kipute cha AFCON ya mwaka 2025.

Katika makundi zilizopangwa timu hizo, angalau zipo katika nafasi ya kwanza au ya pili.Katika kundi J ambapo Harambee Stars ya Kenya ipo, inashikilia nafasi ya kwanza kwa alama nne ikitoshana na Cameroon iliyoko katika nafasi ya pili baada ya mechi mbili kila mmoja.

Zimbabwe inashikilia nafasi ya tatu kwa alama mbili huku Namibia ikishikilia mafasi ya mwisho kwa kupoteza mechi zake zote. Wenyeji wengine wa upana wa Afrika mashariki ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania katika kundi H. DR Congo wanaongoza jedwali la kundi hilo kwa alama sita, Tanzania wakishika nafasi ya pili kwa alama nne.

Ethiopia ni wa tatu kwa alama moja huku Guinea wakifunga jedwali bila alama.Majirani wa Kenya Uganda nao wanaongoza kundi K kwa alama zinazotoshana na Afrika Kusini katika nafasi ya pili.

Congo na Sudan Kusini wanashikilia nafasi ya tatu na nne mtawalia kwa tatu na sufuri kwa mkupuo.

Mechi zaidi ya makundi zitaendelea mwezi Oktoba mwaka huu kwa raundi ya tatu.