Shabiki wa Arsenal mahakamani kwa ubaguzi wa rangi

Muhtasari

• Suhel Ali alitoa matamshi ya dhihaki baaya ya Arsenal kupoteza mechi yake dhidi ya Notiingham Forest msimu jana

Mshambulizi Bukayo Saka
Image: HISANI

Shabiki wa timu ya Arsenal ambaye pia ni mwanafunzi wa sheria katika chuo kikuu cha London anachungulia jela kwa makosa ya kurekodi sauti akimdhihaki mchezaji wa Arsenal Bukayo Saka.

Shabiki huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa jina Suhel Ali alikiri kufanya kosa hilo akisema kuwa alituma ujumbe huyo kwa kuchanganyikiwa na hakulenga kumdhalilisha Saka.

Kwa mujibu wa gazeti moja la Uingereza, sauti ya Suhel Ali iliyosikika mbele ya jaji Briony Clarke, alisema, "Wewe ni nyani - wewe ni 'f***ing' nyani."

Matamshi ya Ali yalijiri baada ya Arsenal kupoteza mechi yake dhidi ya Nottingham Forest mnamo mwezi Mei 20 mwaka wa 2023. Mechi hiyo ilisababisha Arsenal kupoteza taji la EPL kwa Man City na ushindi wa Nottingham Forest kuibakisha kwenye ligi kuu.

Jaji Clarke aliahirisha hukumu ya kesi hiyo hadi tarehe nane Oktoba mwaka 2024."Sitakuhumu leo, lakini sikatai chochote." Alisema jaji Clarke.