Gor Mahia na Police FC waaga mashindano ya bara Afrika

Baada ya kupoteza mechi za mkondo wa pili wa kombe la mashirikisho na klabu bingwa barani Afrika mtawalia

Muhtasari

• Police FC walipoteza kwa jumla ya mabao matatu kwa moja dhidi ya Zamaleck kutoka Misri hivyo kuaga mashindano hayo

• Gor Mahia waliaga mashindano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kubebeshwa gunia la mabao sita kwa 

Image: HISANI

Vilabu vya kabumbu kutoka Kenya Gor Mahia na Kenya Police FC vimeaga mashindano ya shirikisho ya soka Afrika CAF.

Kenya Police FC iliaga mashindano ya mashirikisho ya Afrika siku ya Ijumaa 20, Septemba baada ya kupoteza mechi ya mkondo wa pili kwa kushindwa kwa mabao 2 kwa moja.

Mkondo wa kwanza katika mechi iliyochezewa ugani Kasarasni,Zamaleck ya Misri iliilaza Police FC bao moja kwa nunge kwa hivyo kuongeza matumaini ya kuendelea hatua za mbele kutokana na bao la ugenini.

Baada ya mechi wa mkondo wa pili, Police Fc ilikubali kichapo kingine na Zamaleck itapenya kwenye hatua ifuatayo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3 kwa 1.

Gor Mahia kwa upande wao waliaga mashindano ya klabu bingwa barani Afrika kwa kupokea jumla ya mabao 6 kwa 0.

Mkondo wa kwanza ugani Nyayo jijini Nairobi, Gor Mahia walinyoroshwa mabao matatu komboa ufe na walisafiri kwa mkondo wa pili mnamo tarehe 21,Gor Mahia walicharazwa kichapo sawia na cha kwanza.

Timu hizo mbili sasa zimerejea nchini kuendelea na mechi za ligi kuu nchini kwa msimu wa 2024/25.

Ligi hiyo ya FKF iling'oa nanga tarehe 24 Agosti na kufikia sasa Gor Mahia na Kenya Police FC hawajacheza mechi yoyote.