Chelsea waititiga Barrow mabao 5-0 darajani

Mshambuliaji Christopher Nkunku aisaidia timu ya Chelsea kuipiga Barrow mabao matano huku akifunga mabao matatu kwenye pambano la kuwania kombe la Carabao

Muhtasari

•Chelsea wapata ushindi mkbwa wa mabao matano kwa sifuri wakicheza na timu ya Barrow katika mechi ya kuwania kombe la Carabao.

•Christopher Nkunku alionekana kuwa mwiba baada ya kucheka na wavu mara tatu kwa mpigo na kisha Ferman kujifunga na Pedro Neto kupachika bao la tano na la kwanza akiwa na jezi ya Chelsea.

CHRISTOPHER NKUNKU BALOON CELEBRATION
CHRISTOPHER NKUNKU BALOON CELEBRATION
Image: CHELSEA VS BARROW RESULTS

Timu ya Chelsea usiku wa kuamkia hii leo tarehe 25 septemba,wameipiga timu ya Barrow mabao matano bila jibu na kuendeleza msururu wa matokeo mema msimu huu kwa kuwa wamepoteza mechi moja tuu,katika mashindano yote tangia msimu uanze.

Wana Blues,waliopata mabao yao kupitiam wachezaji Christopher Nkunku aliyepachika mabao matatu,Ferman akijifunga na sajilio mpya Pedro Neto akifunga bao la tano na kuhakikishia vijana hao ushindi muhimu mbele ya mashabiki wa nyumbani.

Vijana hao wa Enzo Maresca,wanazidi kuonyesha kana kwamba wanaweza fanya vyema ikikumbukwa kwamba walipoteza tuu pambano moja dhidi ya mabingwa watetezi Man city katika ufunguzi wa ligi ya Uingereza.

Chelsea ambao wameshinda taji hilo mara 5, sasa wamo mbioni hili anghalabu kulitwaa kwa mara ya sita chini ya kocha mpya Enzo Maresca.

Chelsea walifika fainali makala yaliyopita ya taji hili na kupoteza mikononi mwa timu ya Liverpool bao moja sifuri chini ya ukufunzi wake Mauricio Pochetino.

Barrow ambao ni viongozi wa ligi ya daraja la pili hakuwa na la kufanya katika uga huo wa Stamford Bridge kwa kuzidiwa ubabe na mabingwa hao wa kombe la klabu bingwa ulaya mwaka 2021.

Baada ya ushindi huo mkubwa,kocha Enzo Maresca alisema kuwa walikuwa wanatoa ishara kuwa wana wachezaji wachanga ambao wanaweza kufanya vizuri,baada ya kuanzisha kikosi cha pili katika mechi hiyo.

Kando na Chelsea,matokeo mengine katika taji hilo ni kwamba Manchester City waliipiga timu ya Watford 2-1, Leiceseter city kushinda mabao matatu kwenye matuta ya penati baada ya sare tasa na Walsall, nao Aston Villa wakaipiku timu ya Wycombe 2-1.