Yassine Bounou: Mfahamu kipa nyota wa Morocco mzaliwa wa Canada mwenye lafudhi ya Kiajentina

Aliondoka Morocco aliposajiliwa na Atlético de Madrid

Muhtasari

•Bono amevutia hisia za Kombe hili la Dunia kwa umaarufu mkubwa kama alivyoonyesha kwenye mechi dhidi ya Uhispania.

•Yassine Bouno alizaliwa mbali na Moroco: huko Montreal (Canada). Alirudi katika ardhi ya wazazi wake alipokuwa na umri wa miaka 7.

Image: BBC

Morocco imepata nafasi ya heshima katika Kombe la Dunia la Qatar 2022.

Kwa mara ya kwanza, timu ya Afrika inatinga nusu fainali, baada ya kuilaza Ureno katika robo fainali.

Kufuzu kwake sio tu kushiriki mechi nane bila kupoteza bali kucheza mechi saba bila kufungwa goli, mafanikio ambayo yametokana na kipa wake nyota: Yassine Bouno, anayejulikana zaidi kama Bono.

"Tuko hapa kubadilisha fikra na kuondokana na hali ya hofu," alisema kipa huyo mwenye umri wa miaka 31. "Morocco iko tayari kukabiliana na mtu yeyote duniani, zaidi ya nusu fainali na kitu kingine chochote."

Bono amevutia hisia za Kombe hili la Dunia kwa umaarufu mkubwa kama alivyoonyesha kwenye mechi dhidi ya Uhispania, alipookoa penalti mbili na hakuruhusu bao ndani ya dakika 130. Mchezo huo, ambao uliondoa timu ya Uhispania, ulikuwa hatua ya kihistoria kwa mpira wa miguu wa Morocco.

"Tumebadilisha mawazo haya na kizazi kitakachokuja baada yetu kitajua kuwa wachezaji wa Morocco wanaweza kusababisha miujiza," alisema.

Bono aliokoa penalti mbili kwenye mchezo dhidi ya Uhispania na hakuruhusu bao katika dakika 130
Bono aliokoa penalti mbili kwenye mchezo dhidi ya Uhispania na hakuruhusu bao katika dakika 130
Image: BBC

Kipa huyo, ambaye kwa udadisi ameendeleza sehemu nzuri ya maisha yake huko Uhispania, anatokana na kuwa na jukumu bora kama golikipa wa Sevilla.

Mchezo wake ulimfanya achukuliwe kuwa kipa bora wa tisa duniani kwenye Tuzo ya Ballon d'Or kwa kupokea Tuzo ya Yashin 2022 na kushinda Tuzo yake ya kwanza ya Zamora kama kipa aliyefunga mabao machache zaidi katika msimu wa 21-22.

Bono alikua shujaa wa timu yake mnamo Machi 2021 dhidi ya Valladolid, akifunga bao katika dakika ya 93 na kusawazisha. Kazi hiyo ya golikipa haikuwa imefikiwa kwa muongo mmoja ndani ya Ligi ya Uhispania.

Uchezaji wa Bono katika nusu fainali ya Agosti 2020 pia uliruhusu Sevilla kuwaondoa Manchester United 2-1 na kushinda taji lao la sita la Ligi ya Europa.

Shabiki mkubwa wa Argentina

Yassine Bouno alizaliwa mbali na Moroco: huko Montreal (Canada). Alirudi katika ardhi ya wazazi wake alipokuwa na umri wa miaka 7. Tangu alipokuwa mdogo, alionyesha kupendezwa na soka na alikuwa sehemu ya klabu ya Wydad Casablanca, lakini baba yake alipinga kujitolea kwake katika mchezo huo. Walakini, Bono alisisitiza kuwa mtaalamu.

Aliondoka Morocco aliposajiliwa na Atlético de Madrid. Uzoefu huo haukutoa kile alichotarajia na akakata tamaa. Alihudumu misimu miwili na Zamora (2014-2016) na kisha na Girona (2016-2019). Mpaka akaishia Sevilla.

 Maisha yake yamehusishwa na Uhispania. lakini, inajulikana kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa mpira wa miguu wa Argentina na shabiki wa River. "Jezi ya kwanza niliyopewa na baba yangu ilitoka Argentina," kipa huyo alisema.

Bono anachukuliwa kuwa kipa bora wa tisa duniani baada ya kupokea Tuzo la Yashin 2022.
Bono anachukuliwa kuwa kipa bora wa tisa duniani baada ya kupokea Tuzo la Yashin 2022.
Image: BBC

Uhusiano wa karibu ambao lafudhi yake ya kipekee ya Argentina inahusishwa nayo. "Mimi ni Mmorocco zaidi kuliko kitu kingine chochote. Kinachotokea ni kwamba nilipofika Uhispania nilijifunza na Waajentina na lafudhi yangu ikabadilika kidogo," alielezea mara moja.

Mchezaji anayemwenzi sana ni Ariel Ortega, mchezaji wa zamani wa soka wa Argentina anayejulikana zaidi kama "El Burrito Ortega." Bono alikiri katika mahojiano kwamba mbwa wake anaitwa Ariel, kwa heshima ya mchezaji huyo.

Sasa macho ya dunia yapo Morocco. Glovu za mlinda mlango wao nyota zimesaidia timu ya Afrika kufikia kiwango bora katika Kombe la Dunia, tangu Mexico 86. Je, itakuwa zamu ya Bono kumenyana na timu ya Argentina? Tutaona.