Misri wajiunga na Nigeria katika 16 bora baada ya kubandua DR Congo

misri
misri
Wenyeji Misri walijiunga na Nigeria katika kundi la 16 bora katika kipute cha AFCON  mwaka huu kufuatia ushindi wao wa 2-0 dhidi ya DR Congo katika mechi yao ya kundi A.

Mabao ya Nahodha  El Mohamady na mshambulizi wa Liverpool Mo Salah kunako kipindi cha kwanza yalitosha kuwabandua DR Congo. Kwingineko Uganda walitoka sare ya 1-1 na Zimbabwe na kupanda hadi katika nafasi ya pili wakiwa na alama 4, mbili nyuma ya Misri.

Ifuatayo ni msururu wa spoti duniani.

FIFA imeanzisha michakato ya kinidhamu dhidi ya Cameroon kufuatia kupoteza kwao kwa mabao 3-0 kiutata kwa Uingereza katika michuano ya kombe la dunia la wanawake.

Uingereza ilifuzu kwa robo fainali ya kipute hicho baada ya ushindi huo laiki mechi hio ilighubikwa na utata wa VAR uliopelekea Cameroon kudinda kuanza mara mbili baada ya kuamuliwa kwa mabao dhidi yao na VAR.

Camerron inachunguzwa kwa utovu wa nidhamu na tabia zisizo za sawa.

Juventus wamekubaliana na mlinzi wa Ajax Matthijs de Ligt sheria na masharti ya kumsajili kwa kandarasi itakayompelekea kulipwa zaidi ya pauni million 10 kila msimu.

Juve pia wataweka kandarasi ya zaidi ya pauni million 135 iwapo watamuuza chipukizi huyo anayechezea Uholanzi. Hata hivo PSG ya Ufaransa pia walionyesha nia ya kumsajili, baada ya De ligt kukataa kujiunga na Barcelona.

Huko Uingereza, Manchester United na Crystal Palace wamekubaliana ada ya kitita cha pauni milioni 50 kwa ajili ya Aaron Wan-Bissaka.

Mlinzi huyo kutoka Uingereza mwenye umri wa miaka 21 ataigharimu United jumla ya pauni milioni 45 pamoja na pauni milioni 5 kama marupurupu.

Ni mchezaji wa pili kusajiliwa na United msimu huu wa joto baada ya kusajiliwa kwa Daniel James kutoka Swansea.