Yaya ahukumiwa maisha jela kwa kumbala mvulana wa miaka 6 Rongo
Yaya mmoja huko Rongo amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kumbaka na kumwambukiza maradhi ya zinaa mtoto mvulana mwenye umri wa miaka sita . Neema Matiko mwenye umri wa miaka 22 amepewa hukumu hiyo na hakimu mkuu wa Rongo Raymond Langat kwa kosa hilo alilotekeleza machi tarehe 30 mwaka huu . Langat amesema amempa mtuhumiwa hukumu hiyo kali kwa kutumia vibaya maamaka yake kuhatarisha maisha ya mtoto huyo licha ya kufahamu kwamba alikuwa na maradhi ya zinaa .
Hatutaki kuwatenganisha binti zetu
Mama za wasichana pacha kutoka kakamega wamesema wameshindwa jinsi ya kuwashughulikia binti zao baada ya uchunguzi wa DNA kuthibitisha kwamba watoto hao ni pacha .Rosemary Khaveleli na Angeline Omina hata hivyo wamesema wameamua kwamba hawatawatenganisha wasichana hao kwani hakuna kati yao anayetaka kuishi mbali na mwenzake .
Duka na ufamasia karibu na Hospitali ya Machakos Level Five zafungwa
Gavana wa machakos Alfred Mutua ameongoza msako dhidi ya duka za ufamasia zinazokaribiana na hospitali ya machakos level five ambapo watu 12 wamekamatwa na duka hizo za dawa kufungwa . wamiliki wa duka hizo za ufamasia na maabara za kibinafsi walipewa notisi ya miezi mitatu ili kuzifunga lakini wakapuuza .
Hakuna kisa che Ebola kilichothibitishwa
Hatuna kisa kilichothibitishwa cha ugonjwa wa Ebola nchini .waziri wa afya Sicily Kariuki amesema kundi la wataalam limemfanyia ukaguzi mgonjwa aliyelazwa huko kericho ambaye alisafiri hadi Malaba na Kuthibitisha kwamba ugonjwa huo hauwezi kutambuliwa kuwa Ebola . amesema kama hatua ya tahadhari sampuli kutoka kwa mgonjwa huyo imechukuliwa kufanyiwa vipimo na shirika la KEMRI .
KWINGINEko watu watatu zaidi wametengwa katika wadi maalum katika hospitali ya rufaa ya kericho kufuatia kisa kimoja kinachoshukiwa kuwa cha ugonjwa wa ebola . mume wa mgonjwa aliyelazwa jana na watu wengine wawili waliomsaidia kumpeleka mkewe hospitalini ndio waliotengw akatika wadi ingawaje hawakuwa wameonyesha daalili zinazofanana na za ugonjwa wa ebola .
Usimwajiri mtoto -Ni hatia
Unajitia katika hatari ya kufungwa jela endapo utamwajiri mtoto aliye chini ya umri wa miaka 11 . wakili Wang'oma Mola amesema watoto aghalabu hutumiwa vibaya kwa sababu hawajui haki zao na pia mashartio ya ajira .
Mahakama Kuu ya Eldoret yamnyima mshukiwa wa mauaji dhamana
Mahakama kuu huko Eldoret imemnyima dhamana mshukiwa wa mauaji Nafatali Kinuthia ,aliyeshtakiwa kwa kumwua mwanafunzi wa matibabu Ivy Wangechi . jaji Stephen Githinji amesema mshukiwa amenyimwa dhamana kwa sababu ya usalama wake na pia kuna uwezekano atavuruga ushahidi dhidi yake endapo ataachiliwa huru .
Polisi mmoja hajapatikana tangu shambulizi la Wajir
Afisa mmoja wa polisi hajulikani aliko baada ya gari lao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini na kuwauwa maafisa saba wa polisi huko wajir katika mpaka wa Kenya na Somalia . watatu waliokolewa wakiwa hai ilhali mwingine aliyekuwa ametoweka alipatikana jana .
JSC yaanza kuwaajiri majaji 11
Tume ya huduma kwa idara ya mahakama imeanza kuwaajiri majaji 11 wa mahakama ya rufaa ili kushughulikia upungufu uliosababishwa na kupandishwa vyeo kwa baadhi ya majaji na wengine waliostaafu . majaji 22 na m,awakili 13 wamehojiwa kwa nafasi hizo .
Jopo la kumchunguza Jaji Jacktone Ojwang' Latajwa
Jopo la wanachama saba limeundwa ili kuchunguza mienendo ya jaji wa mahakama ya juu zaidi Jackton Ojwang . wanachama wa jopo hilo ni pamoja na jaji mstaafu Festus Azangalala, Ambrose Weda, Andrew Bahati Mwamuye, Lucy Kambuni, Sylvia Wanjiku Muchiri na Amina Abda. Jopo hilo litasimamiwa na jaji wa mahakama ya rufaa Alnashir Visram na litakuwa na mawakili wawili walioteuliwa na rais Kenyatta kulisaidia katika kazi yake . vikao vitaanza julai tarehe 15
Ruto huenda akapunguza Kampeini za 2022
Naibu wa rais William Ruto huenda akaamua kupunguza kasi au akasitisha kampeini zake kuwania urais mwaka wa 2022 baada ya rais Uhuru kenyatta kukemea vikalia wanaoendelea kupiga siasa . mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Calvin Muga hata hivyo anasem Ruto ana chaguo la kuendelea kufanya kampeini lakini nje ya chama cha Jubilee .
Waagizaji wa magari walalamikia Mombasa walalamikia
Baadhi ya waagizaji wa magari kutoka nje huko Mombasa wanalalamikia hatua ya serikali ya kaunti hiyo kubomoa yadi zao wanazotumia kuyauza magari hayo . wamesema serikali imepuuza agizo la mahakama lililozuia kubomolewa kwa yadi hizo .serikali ya kaunti imedai kwamba yadi hizo zilijengwa kinyume cha sheria .
Mwanamme ampiga mkewe kwa kumpikia wali
Mwanamke mmoja anauguza majeraha mabaya huko Kirinyaga baada ya kudaiwa kuchomwa na mumewe kuhusu chakula . shangazi yake mwathiriwa amesema jamaa huyo alikuwa amemtaka mkewe kumpikia Githeri lakini badala yake mkewe akamatayarishia wali .
Sonko na wabunge wawili waunga mkono wahudumu wa boda boda kupinga bima ya wateja
Wahudumu wa boda boda na tuk tuk wamepata uungwaji mkono kutoka kwa gavana wa Nairobi mike sonko na wabunge wawili katika jitiahada zao za kuzuia pendekezo la serikali kuwataka wawalipie wateja wao bima . wanataka mahakama kuzuia pendekezo hilo kwa wakisema litaongeza gharama yao ya kufanya kazi .
Maafisa wa Kliniki Tana River wagoma
Maafisa wa kliniki huko Tana River wamegoma kulalamikia hatua ya serikali ya kaunti kukataa kusaini mktaba wa kuwatambua na kushughulikia lalama zao . Katibu mkuu wa muungano wao George Gibore amesema serikali ya kaunti ya Tana River imeyapuuza maslahi yao kwa miaka minne
Tuko tayari kukabiliana na Ebola -Waziri wa Afya
Waziri wa afya Sicily kariuki amewahakikishia wakenya kwamba serikali imejitayarisha kukabiliana na ugonjwa wa Ebola .Arifa ya tahadhari kwa maafisa wote wa afya iliyotumwa na wizara ya afya ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa kukabiliana na tishio la virusi hivyo.