Mtindo mpya wa mlinzi wa Harambee Stars Joash Onyango wasisimua wakenya

Mlinzi wa Gor Mahia na Harambee Stars, Joash Onyango amewasisimua wakenya wengi kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha zake kuenea.

Onyango ambaye yuko pamoja na kikosi cha Harambee Stars, Paris, Ufaransa, amepaka ndevu zake rangi nyeupe, mtindo ambao ume waacha wakenya wengi wakizungumza.

Wiki iliyopita, shirikisho la kadanda nchini, FKF, lilichapisha picha na maelezo yake huku wakisema kuwa ana umri wa miaka 26, swala ambalo lilipingwa na wakenya wengi, labda kwa sababu ya sura yake.

Kwa mda sasa wakenya wengi wamekuwa wakimkejeli huku wakidai kuwa kama yeye ana umri wa miaka 26, basi wao wana umri mchanga zaidi.

Jambo hilo linawadia wakati wachezaji wengi kutoka bara la Afrika wamekumbwa na kashfa za kuficha miaka yao halali.

Mtindo wake mpya ambao unaashiria uzee, unakisiwa kuwa namna yake ya kuwakejeli wanao shuku miaka yake.

Kevin Teya alidai kuwa Joash Onyango anafuata mtindo wa ma gwiji wa kombe la mabingwa Afrika, El Hadji Diouf wa Senegal na Rigobert Song wa Cameroon ambao pia waliwahi paka ndevu zao rangi nyeupe.

Kikosi cha Harambee Stars kiko Ufaransa katika kambi ya mazoezi na kitaelekea Misri leo jioni.

Tazama picha zake.