Mungu apewe sifa kweli! Kutana na watu maarufu nchini ambao walikuwa 'Chokoraa'

NA NICKSON TOSI

Watu wengi katika karne ya sasa hutamani sana kuzaliwa katika familia zenye uwezo na wazazi walio na uwezo wa kukithi maslahi yote.

Sio wote ambao ndoto kama hizo hutimia ,kuna wale ambao hupitia katika changamoto na hatimaye kubarikiwa maishani.

Hapa nimekuchorea taswira ya baadhi ya watu ambao walikuwa chokoraa,ama watoto wa kuranda randa mitaani.

Guardian Angel

Ni msanii anayefahamika sana kutokana na nyimbo zake za kuwapa wengi moyo ,na kila mara anapokuwa katika mahojiano na vyomba vya habari mbali mbali ,Guardian hudai kuwa baada ya mamake kufutwa kazi alijikuta katika mitaa ya humu nchini kwani ilimwia vigumu kwa mamake kukimu maslahi yao.

Guardian aidha hutokeza kuwa alitiwa mbaroni na polisi baada ya rais wa tatu wa humu nchini kudai kuwa watoto wote wanaoranda randa mitaani kuondolewa mijini kwani walikuwa wanafanya miji kuonekana michafu.