Mwanaume anakabiliwa na kifungo kwa kumtusi jirani yake 'makalio'

makalio
makalio
Mwanamume mmoja anakabiliwa na kifungo cha miezi sita gerezani au alipe faini ya shilingi elfu 5, baada ya kumtusi jirani yake kwa kumwita 'makalio'.

Mahakama iliambiwa kwamba jamaa huyo Joshua Njeru alimtusi Lucy Gachingi alipokwenda nyumbani kwake kuregesha bidhaa aliyokuwa ameazima, na kumfuata nyuma na kutishia kumdhuru.

Mkusanyiko wa habari humu nchini,

Kuwa makini na usiingize hisia unapozungumzia mdosi wako wa zamani, unapokwenda kwa mahojiano ya kazi mpya. Mtaalamu wa HR Carolyne Gaithuma anasema kumuongea vibaya mdosi wako huenda kukakufanya kupoteza nafasi hio ya kazi, kwani watakuona kama mtu ambaye hawezi kuvumilia wakati mgumu.

Nairobi inachangia idadi kubwa ya wasichana wanaobaleghe walio wajawazito, wa kati ya umri wa miaka 10 na 14, huku ikiwa visa 2,400 viliripotiwa mwaka uliopita.

Ripoti ya baraza la kitaifa la idadi ya watu na maendeleo NCPD inaonyesha kuwa Nakuru inafuatia ikiwa na visa 1,700 ikifuatiwa na Kajiado ambayo ina visa 1,500. Isiolo na Lamu ndio zilizo na idadi ndogo zaidi ya visa 14 na 22 mtawalia.

Kaunti ya Narok inachangia idadi kubwa zaidi ya mimba za wasichana wadogo humu nchini kwa asilimia 40, huku Homabay na Pokot Magharibi zikirekodi idadi ya pili na tatu ya juu zaidi kwa asilimia 33 na 29 mtawalia.

Ripoti ya baraza la idadi ya watu na maendeleo NCPD inaonyesha idadi katika kaunti zingine 19 ni kati ya asilimia 18 na 28.

Unaweza kujipata gerezani au kutozwa faini kwa kusambaza jumbe za uongo kuhusu coronavirus, ikiwa una ufahamu au hauna. Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema unafaa kuchunguza jumbe hizo kabla ya kuzisambaza ili kujua iwapo ni za kweli au la.