Nangoja makamu wa Rais William Ruto anipe pesa nifanye harusi

Ent-Freddie
Ent-Freddie
Mcheshi Fred Omondi alifunguka na kusema kuwa anangoja makamu wa Rais William Ruto agharamie harusi yake.

Fred ambaye kwa sasa hana mpenzi alisema kuwa, makamu wa Rais humpa moyo wa kufunga harusi na kumwomba mheshimiwa ampe pesa kiasi ya kugharamia harusi yake.

Zaidi ya hayo, alisema kuwa yeye hufurahishwa sana na vile ambavyo Makamu wa Rais hutoa mchango kwa ukarimu sana kila wakati, makanisani.

"I am trying to wait for the money Deputy President William Ruto contributes during church harambees to get to me," alisema.

Zaidi ya hayo, Fred alisema kuwa akipewa shilingi elfu mia mbili, (200 000) atafunga ndoa.

"If he gave me just Sh200K, I would do a wedding."

 Vilevile alisisitiza na kusema kuwa, makamu wa Rais ndiye anayemzuia na kumwambia mheshimiwa akohoe tu, kisha afanye harusi.
''DP, you are the one holding me back, just cough so that I can wed," alisema.

Alipoulizwa kama amewahi achwa na mpenzi wowote, alisema kuwa, kuna wakati ambao mpenzi wake alimwacha kwa sababu alikuwa na tabia ya kuongea na wasichana wengi sana wakati wa matukio zake za burudani.

"I was once dumped by a woman because I was too social with ladies during my events."

Hata hivyo, Fred alisema kuwa utenganisho wake na wapenzi wake huwa kwa njia ya utulivu sana na mara kwa mara wanapokata ushirikiano wao wa kimapenzi, wao huenda kuwa marafiki wa dhati.

Kwa sasa, Fred anazingatia Comedy show itakayokuwa kwenye televisheni.