Ripoti hiyo inayongazia athari za kiuchumi na kijamii za janga la corona iliyofanywa na shirika la takwimu nchini imesema asilimia 37 ya watu walishindwa kumudu gharama ya kodi zao mwezi Mei. Utafiti wenyewe ulifanywa mwezi Juni na uliwahusisha watu 14,616 waliohojiwa na imefichua jinsi virusi vya corona vilivyovuruga hali ya kiuchumi na kulemaza kipato cha watu wengi. Kando na kuvuruga mapato ya watu wengi, kuna mengi ambayo watu wamejifunza wakati huu wa janga hilo kama ilivyojadiliwa kwa undani katika Podi hii ya Yusuf Juma
&t=596s
Kulingana na utafiti huo, takriban asilimia 30.9 ya wapangaji ambao hulipa kodi zao ndani ya muda ulioafikiwa na wenye nyumba kabla ya janga la corona walishindwa kulipa kodi zao mwezi Mei.
Ripoti hiyo imeonyesha kwamba asilimia 61 ya waliokosa kulipa kodi zao walitaja kudorora kwa kipato chao kwa ajili ya janga la corona kama sababu ya kushindwa kulipa.
Mapato ya kampuni nyingi yamevurugwa kwa ajili ya janga la corona na kuzilazimu nyingi kuwafuta kazi baadhi ya wafanyikazi.