'Ni wetu!' Wakenya wadai baada ya Mbwana Samatta kusajiliwa na Aston Villa

mbwana samatta
mbwana samatta
Aston Villa wamekamilisha mktaba wa pauni milioni 10 kumsajili mshambulizi wa Genk Mbwana Samatta.

Raia huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 27 ametia saini mkataba wa miaka minne na nusu utakaolingana na kupewa kwake kibali cha kufanya kazi.

Amefungia Genk mabao 10 katika mashindano yote msimu huu ikiwemo bao ugani Anfield dhidi ya Liverpool, katika ligi ya Mabingwa. Atakuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi ya Primia.

Habari hiyo imepokelewa kwa furaha kuu kutoka eneo hili la Afrika Mashariki kwani sio jambo ndogo kuwa na mchezaji ambaye anachezea hiyo inayatambulika kama ligi kuu zaidi duniani.

Mkenya Victor Wanyama anayechezea Tottenham, ndiye mchezaji wa kwanza kutoka humu nchini na pia Afrika Mashariki kuchezea ligi ya EPL.

Wakenya hata hivyo, katika mtandao wa Twitter walikiri kuwa Samatta ni mkenya ila sio wa kutoka Tanzania, huku wakimpongeza kwa kujiunga na Wanyama.

Jambo hilo liliwakera watanzania ambao hawakutaka staa wao ahusishwe na Kenya.

Soma baadhi ya jumbe hizo,

https://twitter.com/JoeKisii/status/1219499804063039488

https://twitter.com/_mainanjoki/status/1219364828785016834

https://twitter.com/iamosward/status/1218069519064870912

https://twitter.com/SirAlexas/status/1219467461164261376

https://twitter.com/opijah/status/1219532670906126337