Not Me: Semenya asema hatotetea taji lake la mbio za Mita 800 Septemba

Mwanariadha wa Afrika kusini Caster Semenya  amesema  hatotetea taji lake la ubingwa wa mbio mita 800 duniani mwezi Septemba kufuatia uamuzi dhidi yake katika kesi aliyowasilisha mahakamani kupinga, kuidhinisha viwango vya homoni ya testosterone miongoni mwa wanariadha wanawake. Mwanariadha  huyo wa  Afrika kusini  hata hivyo amesema "ataendelea kupambana kutetea haki za binaadamu" licha ya "kusikitishwa kwake".

 

Semenya amewahi mara mbili kukata rufaa dhidi ya  sheria za IAAF  zinazomzuia kukimbia bila  kutumia dawa  .Lakini uamuzi unaomruhusu kukimbia sasa umebatilishwa.Semenya anapinga sheria mpya za shirikisho hilo la riadha duniani IAAF zinazomtaka yeye na wanariadha wengine walio na utofuati wa ukuwaji kijinsia (DSD) lazima watumie dawa zinazopunguza homoni za testosterone ili kuweza kukimbia katika mbio za kuanzia mita 400 hadi maili moja au abadili mbio atakazoshiriki.

Semenya alikuwa anaweza kukimbia wakati kukisubiriwa uamuzi wa mahakama ya Uswizi, na akiwa awali alishindwa katika rufaa aliyowasilisha katika mahakama inayoshughulikia mizozo katika michezo (Cas) mnamo Mei.Katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa Twitter, Semenya ameandika muda mfupi uliopita, "Nafsi inayojitahidi haiwezi kuzuilika" baada ya kushindwa katika kesi hiyo.Mnamo Mei, Semenya aliwasilisha rufaa katika mahakama hiyo baada ya kushindwa kushinikiza sheria hizo za IAAF kubatilishwa na Cas.Dorothee Schramm, wakili aliyongoza rufaa ya Semenya aliongeza: "Uamuzi wa jaji hauna athari kwa rufaa yenyewe. Tutaendelea kuifukuzia rufaa ya Caster na kuzipigania haki zake msingi za binaadamu. Mashindano huamuliwa mwisho."