PATANISHO: Awache kunisumbua wanawake ni wengi Kenya!

Bwana George alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Evelyn, akisema kuwa wawili hao walikosana vibaya sana kwani alikuwa anaskia habari kuwa alikuwa na mpango wa kando. Isitoshe, alifanya uchunguzi wake na kuhakikisha alichoambiwa.

George anasema kuwa wawili hao walioana kwa miaka 13 na walitengana mwaka wa 2016 na wawili hao wanaishi maeneo ya Naivasha.

"Nilijaribu tu kufuata nyayo zao na nikawafumania kwa nyumba na yule jamaa. Hapo ndipo tulianza kuvurugana na tukaanza kutusiana kupitia ujumbe mdogo kwa hasira." Alielezea George.

Wawili hao walikuwa wamejaliwa watoto 5 na wote wanaishi na mama yao na tangia mwaka wa 2016 mkewe alimueka kwa blacklist na hawajaweza kuzungumza.

Alipopigiwa simu bi Evelyn hakuzungumza nasi na alisitisha mazungumzo kati yake na bwana George.

"Siwezi zungumza na yeye, sahii ndio anajua kunitafuta juu nimemsomeshea watoto wamekuwa wakubwa, kijana amemaliza form four msichana ako form three hajui hata wanasoma aje na wanakula aje. Akwende huko siwezi ongea na yeye hata afanye nini." Alisema bi Evelyn alipokubali kuzungumza nasi.

Kuhusu mpango wa kando, alisema kuwa hawezi zungumzia swala hilo kwani litamkasirisha na hataki kusumbuliwa. Wanawake ni wengi Kenya mzima, atafute mwanamke aoe apeleke kwao."

Evelyn aliongeza,

"Mimi kama ananitaka angoje kaburi yangu kama anataka akuje achukue kaburi azike lakini mimi najua nitazikwa kwetu. Hakuna msamaha ataniomba ama aende akaombe mamangu kwa kaburi awache kunisumbua."