PATANISHO: Mke Wangu Alikuwa Na Uhusiano Na Mchungaji Ambaye Alifariki Wakishiriki Mapenzi

patanisho
patanisho
Hapo jana, bwana Isaiah kwa unyenyekevu mwingi na upole aliomba apatanishwe na mkewe Wangari ambaye walikosana tarehe 15 Januari mwaka huu, kwani alisema kuwa alikuwa korokoroni na alipowachiliwa alijulishwa kuwa mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchungaji mmoja.

Isitoshe aliarifiwa kuwa mchungaji huyo aliaga dunia wakishiriki kimapenzi baada ya kunywa dawa za kusisimua mwili.

Kulingana na bwana Isaiah "Mimi jioni moja niliona mtu amechukua vitu dirishani akatoweka na pikipiki hata bila kuniarufu. Jambo la kushangaza ni kuwa asubuhi yake alinipeleka matembezi kiasi kiasi akaninunulia kinywaji sasa sielewi ni nini ilitokea. Kitambo mwaka wa 2014 watoto waliniarifu kuwa hawajapikiwa kumpigia simu akanidanganya kuwa yuko nyumbani ilhali nikimuarifu ampatie mtoto simu anakiri kuwa mtoto ameenda kwa jirani. Mwaka uliofuata jambo kama hilo likatendeka tena na kumpigia simu nikama alikuwa kwa kilabu. Nilitoka jela baada ya kufungwa miaka miwili kufika nyumbani niligundua kuwa mke wangu alikuwa na uhusiano wa mapenzi na mchungaji mmoja jambo lililonishtua sana. Siku aliyoninunulia kanywaji alikuwa ananiomba msamaha huku akinielezea kuwa mchungaji huyo alitumia dawa za kusisimua misuli na akafa wakishiriki mapenzi."

Alieleza bwana Isaiah huku akiongeza kuwa baada ya kurudi nyumbani hapo ndipo alimpata mgeni ambaye alikuwa na ufahamu wa yote yaliyotendeka na alipogundua kuwa Isaiah ana uhondo wote ndipo alipoamua kutoweka.

"Alinitishia atanikata na akatishia mamangu pia kwa hivyo nikatoweka ili nimpe mda apunguze hasira zake kwani nilijua angenikata. Licha ya hayo sina ubaya naye kwani akiwa jela nilikuwa namtembelea hadi Machakos jela huku nikiwa nimembebea chakula halafu anadai kuwa nilikuwa na tabia za usherati."

Alisema bi Wangari huku akibubujikwa na machozi.

"Mimi sirudi!" Aliongeza bi Wangari huku akiwa amejawa na hasira baada ya bwana Isaiah kuwa mkali kama simba.

Pata uhondo kamili.