patanisho

PATANISHO: Mke wangu alinisingizia kuwa nilimbaka mjakazi

Frank, 44, ndiye aliyetuma ujumbe hivi leo  akiomba apatanishwe na mkewe bi Beatrice, akisema “Naomba mniokolee ndoa yangu naumia sana.” Aliongeza kuwa alisingiziwa kuwa alimbaka mjakazi wao.

PATANISHO: Mke wangu alinisingizia kuwa nilimbaka mjakazi

Tumekuwa tukiishi vyema kwa miaka 18 na kwa sababu ya kazi nikapelekwa hadi Bomet na kumuacha mke.

Ulifika wakati mke akabadili tabia na kumchunguza nikapata ana mpango wa kando na nikijaribu kumwambia turudiane akaanza vijisababu. Alinisingizia kuwa nina mpango wa kando na pia nilimbaka mfanyikazi wetu wa nyumba.

Frank alisema kuwa alithibitisha kuwa mkewe ana mpango wa kando kwa sababu kuna siku alisema kwamba yeye si baba ya watoto wake, jambo ambalo linamuuma hadi wa sasa.

Frank aliongeza,

“Yeye alikuwa anataka kuni provia ana mpango wa kando kwani sasa hivi amejifungua baada ya kushika mimba nje ya ndoa. Sasa hivi tumetengana na hatuishi pamoja,” alisema.

Hata hivyo licha ya majaribio ya kutaka  kupatanisha, juhudi zetu za kumfikia Beatrice hazikufua dafu.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments