PATANISHO: Wamama ploti wanapotosha mke wangu - Bwana Orina

'Jirekebishe na usisumbue mke wako kwani mambo ya kupiga mke ni kitu ambcho imepitwa na wakati'. Hayo ni maoni ambayo mtangazaji Gidi alimshauri Bwana Orina wakti alipiga simu studio, akiomba patanisho na bibi yake.

Bwana Wycliffe Roni aliomba Gidi aokolee ndoa yake baada ya bi Triza Kemunto kutoroka kwao.

Orina alisimulia kilichotokea:' ni kitambo kidogo Januari, lakini ugomvi ulianaza mwaka jana. tulikuwa tunaulizana kidogo ako na group mbaya inayompatia mawaidha, na nilikuwa nilitaka mtot mwingine lakini nikatambua anatumia tembe fulani alipewa na dakatri wa family planning. Kitu cha tatu ni kuwa anashindanga kwa whatsapp alkini anashugulikia simu tuu, na nikagundua anawhatsapp na mwanaume mwingine. Tangu ya siku hiyo anaweka password kwa simu.

Wakati nilikuwa nimetoka kidogo nilirudi kukuta bibi yangu alitoroka na mtoto wetu.

Orina wa miaka 29, na Trizah wa miaka 26 wamekaa kwa ndoaa miaka sita.

'Saa hii anakaa side hiyo ya kangemi na tunaongea, anakataalia aakisema ashaniondokea, lakini licha ya yote ningependa kumwomba msamaha, turudiane and tutunze mtoto wetu.'

Skiza kanda, uweze kujua kama walisuluhisha hii mambo.