Pesa Otas! Vihiga United yasajili wachezaji 10 wapya

vihiga united
vihiga united

Timu ya National Super League Vihiga United imewasajili wachezaji kumi wapya ili kuboresha kikosi chake huku wakipania kurejelea katika ligi kuu ya KPL.

Timu hiyo ambayo inadhaminiwa na serikali ya kaunti ya Vihiga pia iliwaachilia wachezaji 16 na kubaki na wengine 15 waliokuwa msimu uliopita.

Rais wa klabu hiyo, Bwana Kahi Indimuli alisema walichukua hatua hiyo ili kuweza kurujesha hadhi katika klabu hiyo baada ya kusushwa ngazi kutoka ligi ya KPL msimu uliopita.

Vihiga ilipandishwa ngazi mwaka wa 2017, miaka minne tu baada ya kuundwa na waliweza kukaa katika ligi kuu kwa misimu miwili lakini walilemewa kujizatiti katika ligi kuu.

“Timu ambayo tumekusanya imepewa jukumu moja kuu, kuturejesha katika ligi kuu humu nchini. Ikifikia mwisho wa mwaka, hatutaki vijisababu vya kwa nini timu haijatekeleza jukumu lao.

Twataka kuwa tukizungumza kuhusu mipango ya kuturudisha katika ligi kuu." Alisema Indimuli alipo ongea na wanahabari wa KNA Jumanne huko Mbale.

Timu hiyo ilimteua Sammy Okoth kama kocha wake. Anachukua usukani kutoka kwa Mike Mururi aliyekuwa kaimu kocha.

Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa ni Peter Joma kutoka Zoo Youth FC, Hillary Otieno kutoka from AP Nairobi, Richard Swegenyi kutoka Vihiga Sportiff, Kelvin Okinda kutoka AP Nairobi na Morgan Abuko from Chemelil.

Wengine ni kama; Kelvin Opiyo kutoka Thika United, Leslie Otieno kutoka Kariobangi Sharks Youths, Mark Owino kutoka Kenyatta University, Abisalom Onyango kutoka Migori Youth na Michael Odongo kutoka Thika United.