Phillipe Coutinho akamilisha uhamisho kwenda Bayern Munich ya Ujerumani

Phillipe Coutinho ameamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani akitokea Barcelona ya Uhispania kwa msimu mmoja.

Bayern inatarajiwa kulipa dhamani ya millioni nane kwa msimu huu huku pia kukiwa na uwezekano wa kumnunua Coutinho kwa ada ya millioni mia moja na ishirini msimu ujao.

 Phill Coutinho alijiunga na Barcelona mwezi januari mwaka 2018 akitokea klabu ya Liverpool kwa ada ya millioni mia moja na arubaini na mbili.
Ndani ya mwaka mmoja na nusu ugani Camp Nou,Coutinho alicheka na wavu mara 21 ndani ya mechi 75. Ujio wake Antoine Griezmann umekuwa sababu kuu kwa uhamisho wake Coutinho.
 
Kwingineko ni kuwa aliyekuwa mshambulizi wa AC Milan na Manchester City, Mario Balotelli amejiunga na klabu ya Brescia kwa mkataba wa miaka miwili.
Balotelli mwenye umri wa miaka 28 anatarajiwa kuisaidia klabu hio kufanya vyema msimu ujao kwenye ligi kuu nchini italia.