PICHA: Gwiji wa Liverpool Mo Salah azuru Kenya

Gwiji wa Misri na Liverpool, Mohammed Salah almaarufu Mo Salah anaaminika kuwa nchini Kenya ambapo anapaniwa kujivinjari kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza.

Salah yumo nchini kujivinjari wiki chache tu baada ya nchi yake, Misri kubanduliwa nje katika awamu ya kumi na sita bora katika kipute cha AFCON.

Misri ambao ndio walikuwa wenyeji wa mashindano hayo, walikuwa wamepigiwa upato kushinda taji hilo wakiongozwa na nahodha Salah, lakini wana Afrika kusini walikuwa na maoni tofauti.

Algeria ndio waliotwaa taji hilo kwa mara ya pili baada ya kupiga Senegal kwa bao moja bila jibu.

Inaaminika Mo Salah alikuwa nchini kwa mda mfupi sana alipotembelea hoteli moja jijini Nairobi kabla ya kuendeleza safari yake hadi nchi nyingine.

Mo Salah alikuwa na msimu wa kufana na klabu yake ya Liverpool ambapo alishinda taji la Champions League baada ya kumaliza wa pili kwenye ligi kuu, nyuma ya Manchester City.

Hata hivyo, alikuwa miongoni mwa wafunga bao bora kwani alitikisa nyavu mara 22 mabao sawa na mwenzake Sadio Mane na Pierre-emerick Aubameyang wa Arsenal.

Tazama picha ifuatayo.