[PICHA] Maandalizi ya Kipchoge Vienna kabla ya Ineos1:59 Challenge

Bingwa wa Olimpiki katika mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge ambaye aliondoka kwenda Vienna ndani ya jeti la kifahari aina ya Gulfstream G280, amesema ana matumaini sana ya kuvunja rekodi hiyo anayotarajiwa kukimbia mbio hizo kwa chini ya saa mbili wikendi.

Baada ya kuwasili, Eliud Kipchoge alianza siku yake ya kwanza huko Vienna kwa kufanya mazoezi ya mbio hizo pamoja na wanariadha wenzake wa pembeni.

Kipchoge ambaye alifika Vienna Jumanne  alionekana mchangamfu huku akianza maandalizi hayo kwa kufanyia mwili wake mazoezi maalum ana kunyosha viungo.

Anatazamiwa kuvunja rekodi yake katika mbio za masafa marefu kwa chini ya saa mbili maarufu kama INEOS 1:59 Challenge alipewa hadhi ya hali juu sana na bwanyenye Sir Ratchliffe ambaye anafadhili mbio hizo.

Nimefurahiya sana kuwa hapa Vienna. Kwa sasa nimeona kozi hiyo kwa mara ya kwanza na inaonekana kuwa nzuri, "Kipchoge alisema.

"Nina hamu sana ya kushiriki mbio hizi na ni matumaini yangu kuwaona wote wikendi hii." Kipchoge alisema.